Tetesi za soka Ulaya Mbappe, Pogba, Bellingham, Henderson, Ekitike, Neves

Juventus itafanya mazungumzo mapya na wawakilishi wa Manchester United na kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 29, Jumatatu. (Mirror)

Newcastle wamezidisha nia yao ya kumchukua mlindalango wa Manchester United na England Dean Henderson, 25. (Mirror)

 

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe

 

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, anasema yuko ''karibu'', kufanya uamuzi juu ya hali yake ya baadaye na atatangaza ''hivi karibuni kabisa''baada ya kuhusishwa na uhamisho wa kuondoka katika Paris St-Germain. (Get Football News France)

 

Barcelona wanakaribia kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Wolves na Ureno Ruben Neves, 25. (Sport - in Spanish)

 

MATANGAZO

Newcastle wanamtaka mshambuliaji wa Reims Hugo Ekitike, 19, lakini Borussia Dortmund pia wanatafakari iwapo watamchukua Mfaransa huyo kukaba nafasi ya Erling Haaland. (Fabrizio Romano)

 

Liverpool wako mstari wa katika kinyang'anyiro cha kusaini mkataba na kiungo wa kati wa timu ya vijana wadogo ya Birmingham Jobe Bellingham, 16, kaka yake mchezaji wa kimataifa wa England Jude Bellingham. (Mirror)

 

Arsenal wanaangalia uwezekano wa kumuuza kiungo wa kati-nyuma Mbrazili Gabriel

 

Arsenal wanaangalia uwezekano wa kumuuza kiungo wa kati-nyuma Mbrazili Gabriel

 

Arsenal wanaangalia uwezekano wa kumuuza kiungo wa kati-nyuma Mbrazili Gabriel, 24 huku Juventus wakiwa na nia na mchezaji huyo. (Tuttosport - in Italian)

 

Mchezaji maarufu wa Denmark Christian Eriksen, 30, ambaye kwa sasa ana mkataba wa muda mfupi na Brentford, anasema "angependa kucheza katika soka ya championi Ligi pia" huku akitafakari hali yake ya usoni kwa ajili ya msimu ujao . (Viaplay via Football365)

 

Meneja wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino

Meneja wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino

 

Meneja wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino yuko tayari kukutana na rais wa klabu Nasser Al-Khelaifi huku kukiwa na tetesi kuhusu hali yake ya baadaye . (Marca - in Spanish)

 

Rais wa heshima wa Bayern Munich Uli Hoeness anaserma madai ya mshambuliaji Robert Lewandowsk kwamba hatasaini mkataba mpya "yote ni kuhusu pesa" na anaimani Mpoland huyo mwenye umri wa miaka 33atabakia katika klabu hiyo msimu huu.(Kicker - in German)


Kinglayz Wakuchana

378 Blog posts

Comments