Tanzania yatangaza nyongeza ya mishahara kujibu kilio cha wafanyakazi

MishaharaKima chini cha mshahara kwa wafanyakazi nchini Tanzania kimepanda kwa asilimia 23.3%. Taarifa ya Ikulu imesema.

Tanzania yatangaza nyongeza ya mishahara kujibu kilio cha wafanyakazi

Mishahara

MalundeCopyright: Malunde

Kima chini cha mshahara kwa wafanyakazi nchini Tanzania kimepanda kwa asilimia 23.3%. Taarifa ya Ikulu imesema.

 

Taarifa hiyo iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Zuhura Yunus, imesema Rais Samia Suluhu ameridhia mapendekezo ya nyongeza hiyo mshahara yaliyowasilishwa Ikulu, ikiwa ni muendelezo wa kikao cha waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyepokea taarifa ya wataalamu mjini Dodoma kuhusu nyongeza ya mishahara.

 

'nyongeza hiyo imefanyika kwa kuzingatia Pato la Taifa (GDP), mapato ya ndani yanayotarajiwa kukusanywa katika mwaka 2022/2023 na hali ya uchumi wa ndani na nje ya nchi', ilisema taarifa hiyo.

 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, serikali inatarajiwa kutumia shiligi trilioni 9.7 kwa ajili ya kugharamia malipo ya mishahara ya watumishi wote wa serikali Kuu, Serikali za Mtaa, Taasisi na Wakala za Serikali.


Kinglayz Wakuchana

378 Blog posts

Comments