Unajua kimo chako kinaweza kukuweka kwenye hatari ya kupata magonjwa ?

Kwasasa wastani wa urefu wa watu duniani umeongezeka

Kuna mabadiliko makubwa ya urefu wa watu duniani leo ukilinganisha na enzi za mababu zetu, kwa sasa wastani wa urefu wa watu umeongezeka kulinganisha na miaka 1,00 iliyopita na moja ya mambo yaliyochangia hilo ni kuboreka kwa ma

Watu leo ni warefu zaidi, kwa wastani, kuliko mababu zao miaka 100 iliyopita. Hii ni kweli kwa kila nchi duniani. Lakini ni kiasi gani urefu wa binadamu umebadilika, na hii inatofautianaje duniani kote?

 

Utafiti wa kimataifa uliochapishwa na mtandao wa wanasayansi wa afya duniani, NCD-RisC mwaka 2016 unaonesha wastani wa urefu kwa wanaume duniani umeongezeka kutoka sentimita 162 mpaka 171 na kwa wanawake umeongezeka kutoka sentimita 151 mpaka 159

 

Mtandao wa onhealth.com unabainisha kuwa lishe duni na magonjwa wakati wa utoto hupunguza ukuaji wa binadamu. Matokeo yake, urefu wa wastani wa idadi ya watu unahusiana sana na viwango vya maisha katika jamii husika.

 

Yafuatayo ni magonjwa ambayo mbali na sababu nyingine, kimo chako kinaweza kuhusishwa nayo, ama ukawa kwenye hatari kubwa ya kupata kuliko mwenye kimo tofauti na chako.

 

Saratani

Kwa mujibu wa mtandao wa masuala ya kitabibu webMD.com unaoratibiwa na watabibu nguli, utafiti unaonesha kuwa ukiwa chini ya wastani wa kimo ama urefu wa wastani wa sentimina 171 kwa mwanaume na 159 kwa mwanamke unakuwa kwenye hatari ndogo ya kupata magonjwa hasa saratani.

 

Mgonjwa wa saratani akiwa kitandani

 

Utafiti uliofanywa kwa wanawake 100,000 Ulaya na Makerani ulionesha kwamba, wanawake wafupi walikuwa kwenye hatari ndogo ya kupata saratani ya ovari inayoathiri mfumo wa uzazi.

 

Utafiti mwingine uliofanywa uliohusisha wanaume wa 9,000 Uingereza wenye umri wa kati 50 na 69 ulionesha kwamba wanaume wafupi walikuwa kwenye hatari ndogo ya kupata saratani ya tezi dume.

 

Kisukari

Kwa mujibu wa wafiti, urefu wa miguu yako unahusishwa na uwezekano wa kupata ugonjwa wa kisukari cha aina ya pili. Kwa mujibu wa takwimu za miaka mitano zilizohusisha watu wazima 6,000 watafiti wanaona kwamba watu warefu wako kwenye hatari ndogo ya kupata ugonjwa huo kuliko wafupi.

 

Vifahamu vyakula ambavyo vikichanganywa hugeuka sumu

 

Mgonjwa alivyowashangaza madaktari kwa kuwa na damu yenye rangi nyeupe

 

Ingawa kisayansi haiko wazi kwa namna gani urefu wa miguu unahusishwa na kisukari, lakini kinachoelezwa ni kukihusisha na lishe, kwamba ufupi kwa kiwango kikubwa kunahusishwa na lishe duni wakati wa ujauzito wa mama, matatizo wakati wa kujifungua ama lishe duni wakati wa utoto.

 

Magonjwa ya moyo

Katika hili wanasayansi wanaumiza kichwa kutafuta sababu za kisayasi kwanini hili linawezekana. Walichokibaini ni kuwa watu wafupi wenye kimo cha futi 5.3 wako kwenye hatari kubwa kwa asilimia 50% ya kupata ugonjwa wa moyo kuliko watu wenye urefu wa futi 5.8 au zaidi ya urefu huo.

 

Maradhi ya moyo

Wanachokiona sasa wanakihusisha na lishe duni ama maambukizi wakati wa kujifungua kwa mama kulikoathiri ukuaji wa mtoto.Inawezekana pia kwa mujibu wa wanasayansi kwamba jeni za binadamu zinaathiri kimo chako na kukuweka katika hatari ya kupata matatizo ya magonjwa ya moyo katika maisha yako.

Kupooza

Mtandao wa kitabibu wa webmd.com unasema hili linatokea wakati mtitiriko wa damu inayoingia kwenye ubongo kuathiriwa ama kutokwenda kabisa. Watu warefu wako kwenye hatari ndogo ya kukutwa na tatizo hili kuliko watu wafupi, na linawezekana zaidi kama watu hawa warefu watakuwa na uzito unaotakiwa kiafya.

 

Lishe na masuala mengine ya kiafya wakati wa ukuaji wako kunaweza pia kuathiri urefu wako wa leo na ikachangia katika tatizo la kupooza wakati fulani katika maisha yako.

 

Kuganda kwa damu

Wakati huu wa janga la Corona, kumekuwa na dhana ya baadhi ya chanjo kusababisha damu kuganda. Athari za kitafiti zinaendelea kufanywa katika visa vichache na vya nadra vilivyotokea kuhusu kuganda kwa damu kwa baadhi ya chanjo za Corona.

 

Kuganda kwa damu ni tatizo kubwa na linapohusisha moja ya mishipa mikubwa iayokwenda kwenye mapafu.

Damu

Watafiti mpaka sasa wanashindwa kubainisha kwanini urefu unahusisha na kuganda kwa damu , lakini utafiti unaonyesha unapokuwa mfupi zaidi, uakuwa kwenye hatari ndogo ya kupata tatizo la damu kuganda kwenye mishipa. Watu ambao wanaurefu wa futi 5 au chini ya hapo wako kwenye hatari ndogo kuliko wale wenye urefu wa zaidi ya futi 5.

 

Muhimu kufahamu, magonjwa ama matatizo tajwa yanaweza kusababishwa na mambo mengine ama sababu nyingine zaidi ya urefu ama ufupi wako, lakini kisayansi kimo chako kinaweza kuwa moja ya sababu ya tatizo moja wapo kati ya yaliyotajwa katika Makala hii


Kinglayz Wakuchana

378 Blog posts

Comments