HISTORIA YA ALEXANDER MASHUHURI WA UGIRIKI

Alexander III wa Macedon (20/21 July 356BC-10/11 June 323BC), alijulikana kama Alexander the Great, alikuwa Mfalme wa Ugiriki falme ya Macedon na pia mmoja wa wanafamilia wa family ya Kifalme ya Ugiriki (Agead dynasty). Alizaliwa mjini Pella mwaka 356 BC, Alexander alimrith baba yake Phili

Katika ujana wake, Alexander alikuwa mwanafunzi wa mwanafilosofa Aristotle mpaka kufikia umri wa miaka 16. Aristotle ni mwanafilosopher ambae kanuni zake za ethics bado zinatumika katika ulimwengu wa leo, katika masomo Alexander aliyosoma ilkiuwa ni pamoja na biology, zoology, physics, logic na mengineyo. Baada ya kuuwawa kwa baba yake Philip 336 BC, Alexander alimrithi pamoja na jeshi lenye nguvu na uzoefu. Alexander alipewa cheo cha Generali wa Ugiriki na alitumia cheo chake kuamrisha mipango ya misafara ya kijeshi ya iliyopelekea kushinda na kuiteka Persia. Mnamo mwaka 334 BC, alivamia Ufalme wa Achaemenid ambao ndiyo Cyprus ya sasa, na alianza mipango ya mashambulizi ambayo yaliendelea kwa miaka kumi. Kufuatia kutekwa kwa Asia Ndogo ambayo ni Byzantine (Uturuki) na Anatolian peninsula, Alexander alivunja nguvu ya Persia katika mashambulizi ya mfululizo, mapigano inayosadikika yalivuma sana ya Issus na Gaugamela. Alimtoa mfalme wa Persia Darius III madarakani na alifanikiwa kuuteka ufalme wa Achaemenid na vyote vilivyokuwa ndani yake. Hii ilimaanisha ufalme wake ulianzia Bahari ya Adriatic (Italian Pennisula) mpaka Mto Indus (South Asia, Tibet).

 

Alidhamiria “kufikia mwisho wa dunia na Mwisho wa Bahari Kuu”, aliivamia India 326 BC, lakini ilibidi arudi kwa kuwa askari wake walikumbuka mno nyumbani. Alexander alifia Babylon mwaka 323 BC, mji ambao alipanga kuweka makao yake makuu, bila kuongoza mingango mingi ya mapigano ambayo yalidhamiria kuteka eneo lote la Uarabuni.

Kufuatia kifo chake, mashambulizi mengi sana yaliukumba ufalme wake na kuufanya ugawanyike kuwa nchi iliyomilikiwa na Diadochi, walirithi madaraka ya Alexander.

 

Alexander atakumbukwa kwa mambo mengi ikiwepo la kuweka mwingiliano wa tamaduni katika himaya yake, kama vile Greco-Buddhism. Alivumbua miji 22 na akaipa jina lake, ukiwemo Alexandria uliopo Egypt. Ufalme wa Alexander Ugiriki ulipelekea kusambaa kwa mila za Kigiriki na ilipelekea utaaarabu wa Hellenic, vitu hivi bado viliendelea katia mipito ya Ufalme wa Byzantine katika karne ya 15, na jamii kubwa ya watu wanaoongea Kigiriki katikati na mashariki ya Anatolia mnamo 1920. Alexander alikuja kujulikana kama mwanzilishi na shujaa katika uwiano wa Achilles, na alitokea kama mtu muhimu kwenye historia na tamaduni za Ugiriki na ambazao pia si za Kigiriki. Alikuwa kiongozi ambae viongozi wa kijeshi wamekuwa wakijifananisha nae na pia vyuo vya kijeshi dunia nzima bado wanafundisha mbinu zake za kivita.

 

Maisha ya Awali.

Alexander alizaliwa siku ya sita katika mwezi Hekatombaion hili ni jina moja wapo la miezi ya kihistoria ya kigiriki ambayo inakadiriwa kufananishwa na 20 July BC, ingawa tarehe ina utata, alizaliwa katika mji wa Pella ambao ulikuwa mku mkuu wa Ufalme wa Macedon. Alikuwa mtoto wa mfalme wa Macedon, Phillp II, na mke wake wane aliyeitwa Olympias, alikuwa binti wa Neoptolemus I, mfalme wa Epirus ilyopakana na Italy ya sasa. Ingawa mfalme Phillip alikuwa na wake kati ya saba au nane, lakini Olympias alikuwa mke mwenye madaraka nah ii ilikuwa sababu kubwa ya kuwa mama wa mrithi wa mfalme.

 

Kumbukumbu nyingi zinazonguka kuzaliwa na utoto wa Alexander. Kutokana na mwanahistoria wa zamani wa Kigiriki wa uandishi wa maisha ya watu Plutarch, Olympias, usiku wa kuamkia kufunga ndoa na Phillip aliota kuwa tumbo lake lilipigwa na radi, na ilisababisha cheche za moto kuenea kwa mapana na marefu kabla haijakufa. Kuna wakati baada ya ndoa yao, Phillip alisema, amejiona mwenyewe akilifunga tumbo la mke wake na uzio wenye picha ya simba. Plutarch alitoa maelezo mengi kama tafakari ya ndoto hizi: kuwa Olympias alikuwa na mimba kabla ya ndoa na inaonyeshwa kwa Phillip kufunga tumbo lile; au baba yake Alexander alikuwa Zeus (mungu wa anga na radi). Wanahistoria waligawanyika kimawazo kuhusu uwezekano wa Olympias aliisambaza hadithi ya Alexander kama mzaliwa wa ajabu, wengine wanasema alimwambia Alexander hivyo na wengine wanadai alipingana na mawazo yao kama vile dhambi.

 

Siku Alexander anazaliwa, mfalme Phillip alikuwa najiandaa kwenda kuteka mji wa Potidea ambao ulikuwa kwenye peninsula ya Chalcidice. Siku ileile, Phillip alipata habari kuwa generali wake Parmenion alishindwa na jeshi la pamoja la Illyrian na Paeonian, na pia alipata habari ya kuwa farasi wake ameshinda katika mashindano ya Michezo ya Olympic. Ilifahamika pia kuwa siku hii Nyumba ya Ibada ya Artemis iliyokuwa Ephesus, ambayo ni moja ya Maajabu Saba ya Dunia , imeungua moto. Hii ilipelekea Hegesias wa Magnesia kusema kuwa iliungua kwasababu Artemis alikuwa mbali akisaidia uzazi wa Alexander. Historia hii inasadikika ilitoka wakati Alexander alipokuwa mfalme, na pengine aliileta na kuisisitiza mwenyewe hadharani, kuonyesha watu kuwa yeye hakuwa binadamu wa kawaida.

 

Katika miaka yake ya mwanzo, Alexander alilelewa na nesi, Lanike dada wa atakaekuwa generali wa Alexander baadae Cleitus the Black. Baadae katika utoto wake, Alexander alifundishwa na mwalimu mkali nidhamu aliyejulikana kama Leonidas, ambaye alikuwa ndugu wa mama yake, na pia Lysimachus wa Acarnania (hawa ni watu waliokuwa na ukaribu na familiya ya mfalme na walipewa kazi ya kufundisha watoto wa kifalme). Alexander alikuwa na tabia na desturi za vijana wa Macedonia, alijifunza kusoma, kucheza, kuendesha farashi, kupigana, kuwinda na lyre.

 

Alipofikisha umri wa miaka kumi, mfanyabiashara kutoka Thessaly alimletea mfalme Philp farasi, farasi huyu aliuzwa kwa talanta 13. Farasi huyu hakutaka kukaliwa wala kupewa amri na Phillip aliamrisha atolewe na apelekwe mbali. Alexander hatahivyo aligundua kuwa, farasi yule anaogopa kivuli chake mwenyewe, na aliomba amfundishe farasi yule na alifanikiwa. Plutarch alielezea kuwa Phillip, alifurahi mno kwa kiwango kile cha ushujaa, ujasiri, kutokata tamaa mtoto wake alichoonyesha na kwa machozi alisema “Mwanangu, unahitaji kupata ufalme mkubwa wa kutosha moyo wako wa kutokata tamaa, Macedon si kubwa ya kukutosha”. Na alimnunulia farasi yule, na alipewa jina la Bucephalas maana yake “kichwa cha ngo’mbe”. Bucephalas alimpeleka Alexander nchi za mbali mpaka India. Mnyama yule alipokufa (kwa uzee, Plutarch anasema alikufa akiwa na miaka 30), Alexander aliupa mji mmoja jina la Bucephala.

Maisha ya ujana na Elimu.

Alexander alipofikisha umri wa miaka 13, Phillip alianza kumtafutia mwalimu, aliwafikiria walimu mashuhuri wa wakati huo kama Isocrates Speusippus, alituma barua ya kuwataka waache shughuli zao ili kuchukua jukumu hilo. Baadae Phillip alimchagua Aristotle na alipewa Temple ya Nymphs iliyokuwa mjini Mieza kama darasa. Katika malipo ya ualimu huo Phillip alikubali kuujenga mji wa Aristotle ambao ulikuwa ni mji wa Stageira, Phillip aliujenga mji ule na aliujaza watu ambao walikuwa watumwa walioachwa huru au walioombewa msamaha.

 

Mieza ilikuwa shule ya boda kwa Alexander na watoto wengine wa watu mashughuli wa Macedonia, miongoni mwa watoto hao alikuwepo Ptolemy ambae alikuja kuwa generali wa Alexander na mtawala wa Egypt, Hephaistion ambae alikuja kuwa rafiki wa karibu wa Alexander na kupewa siri nyingi, na Cassander ambae alikuja kuwa mfalme wa Macedonia baadae. Marafiki wengi aliokuwa nao katika shule hiyo baadae walikuja kuwa magenerali wake na kigrup chao kilijulikana kwa jina la ‘companion’. Aristotle aliwafundisha Alexander na companions juu ya madawa, phylosophy, morals, dini, logic na sanaa. Chini ya mafunzo ya Aristotle, Alecander aliijenga mapenzi na kazi za mtunzi wa mashairi aliyeitwa Homer hasa utenzi wake wa Iliact. Aristotle alimpa kitabu chake na alikuwa anakibeba kila alipokwenda.

 

Kuanza kwa umashughuli na kuongezeka kwa Dola ya Macedonia.

Alipofikisha umri wa miaka 16, elimu ya Alexander chini ya mafunzo ya Aristotle ilimalizika. Phillip alianzisha vita na Byzantion (Uturuki ya leo) alimuachia Alexander madaraka ya kuongoza serikali na mrithi kama chochote kikitokea wakati Phillip hayupo, kundi wa wazungu la Thracia Maedi lilivamia Macedonia. Alexander alijibu mashambulizi haraka sana na kuwatoa nje ya eneo lao. Alitawala Ugiriki na kuanzisha mji alioupa jina Alexandropolis.

 

Wakati Phillip anarudi, alimtuma Alexander na jeshi dogo kumaliza ugomvi sehemu ya kusini Thrace. Kampaigni dhidi ya mji wa Ugiriki wa Perinthus, Alexander inasemekana aliokoa maisha ya baba yake. Wakati huo mji wa Amphissa ulianza kuifanyia kazi ardhi iliyobarikiwa na Apollo karibu na Delphi, baraka ambazo zilimpa Phillip nafasi ya kuingilia mipangilio ya Ugiriki. Bado ikimilikiwa na Thrace, aliamrisha Alexander kuanzisha mashambulizi ya kuichukua Ugiriki. Akiwa na wasi wasi kuwa, dola nyingine za Ugiriki zitaingilia, Alexander aliifanya ionekane kama alikuwa anajiandaa kuishambulia Illyria badala yake. Wakati wa machafuko hayo, Illyrians walishambulia Macedonia, na walipigwa vibaya na Alexander.

 

Phillip na jeshi lake walimuunga mkono mwanae mwaka 338 BC, na walitembea kusini kupitia Thermopylae, walipitia mashambulizi mengi kutokea Theban garrison. Waiiteka Elatea, kwa siku chache na kutembea kutona Athens na Thebes. Athens iliongozwa na Dmothenes, na alichagua kutafuta marafiki atakaoshirikiana nao kuishambulia Macedonia. Wote wawili Athens na Phillip walituma wawakilishi kushinda shindano la Thebes, lakini Athens alishinda shindano hilo. Phillip alitembea katika Amphissa (akitekeleza amri ya kikosi cha Amphictyonic hii ilikuwa dini ya zamani sana) walikamata askari wa kulipwa waliotumwa kule na Demosthenes na kukubali kutii amri. Phillip alirudi Elatea, alituma makubaliano ya mwisho ya amani kwa Athens na Thebes, wote wawili walikataa.

 

Phillip alitembea kusini na washindani wake walimzuia karibu na Chaeronea, Boeotia. Katika kipindi hiki vita ya Chaeronea, Phillip aliamuru msaidizi wake na Alexander waondoke na waliongozana na kundi la magenearali walioaminiwa na Phillip. Kutokana na habari za zamani, pande mbili hizo zilipigana mapigano mabaya kwa muda. Phillip kwa makusudi aliyaamuru majeshi yake yasimamamishe mashambulizi na kuhesababu jinsi ya kuwashambulia askari wa hoplitesto (askari wa jani) kwa kuvunja mstari wao. Alexander alikuwa wa kwanza kuvunja mstari, akifuatiwa na magenerali wa Phillip. Walivunja utaratibu wa adui yao hivyo Phillip aliamrisha majeshi kwenda mbele haraka na kuwatangulia. Athens alishindwa vita na Theban alizingirwa na kuachwa apigane mwenyewe. Wote wawili walikua wameshindwa.

Baada ya ushindi huo wa Chaeronea, Philip na Alexander walitembea katika mwelekeo tofauti kuelekea Peloponnese, walikaribishwa na watu wa miji yote; hata hivyo walivyofika Sparta, walikataliwa, lakini hakukutokea mapigano. Corinth, Philp aliweka Utaarabu wa Hellenic (Ustaarabu huu ulirekebisha ustaarabu wa awali wa Persia ambao ulisababisha Vita ya Greco-Persia), ulijumuisha miji mingi ya Kigiriki ukiondoa Sparta. Phillip alipewa jina la H Hegomon likimaanisha Kamanda Mkubwa kabisa kwa wakati huo. Alitangaza pia mipango yake ya kuvamia na kupiga Ufalme wa Persia.

 

Ukimbizini na kurudi.

Wakati Phili anarudi Pella, moyo wake ulikufa katika penzi la Cleopatra Eurydice, ambae alikuwa mpwa wa generali wake Attalus. Ndoa hii ilihatarisha nafasi ya Alexander kama mrithi wa mfalme, ukweli hasa ni kuwa mtoto wa Cleopatra Eurydice angekuwa na nafasi kubwa ya kuwa mrithi wa ufalme wa Macedonia, wakati Alexander alikuwa na nusu tu ya damu ya Macedonia. Wakati wa chakula katika sherehe za harusi hiyo, Attalus akiwa amelewa alisali hadharani kuwa, muunganiko huo ulete mrithi halali.

“Wakati wa harusi ya Cleopatra, ambae Philip moyo wake ulibobea katika penzi lake, na alikuwa bado binti mdogo kwake, mjomba wake Attalus katika manuizi ya kinywaji chake alinuia miungu ya Macedoni iwasikie kupata mrithi halali wa ufalme kupitia mpwa wake. Maneno hayo yalimkasirisha sana Alexander na alimrushia bilauri kichwani.

“Wewe shetani” alitamka Alexander “unamaanisha mimi ni haramu?” Philip alirudi upande wa Attalus, aliamka ili akabiliane na mwanae, bahati nzuri kutokana na mvinyo aliokuwa amekunywa mguu wake uliteleza na alianguka chini. Alexander alimwangalia kwa hasira na kutamka “muone” mwanaume anaeandaa urithi utoke Ulaya kwenda Asia, anaegeuka kutoka kiti kimoja kwenda kingine”

_Plutarch, alivyoelezea ugomvi kati ya Phillip na Alexander.

Alexander alikimbia Macedonia akiwa na mama yake, akiwa ambeba pamoja na kaka yake Mfalme Alexander I wa Epirus ya Dodona, mji mkuu wa Molossians. Aliendelea na safari kuelekea Illyria, ambako alikaa kama mkimbizi kwa hisani ya mfalme wa Illyrian na alikaribishwa kama mgeni, pamoja na kuwa walikuwa wamewashinda kwenye vita. Pamoja na yote yaliyotokea lakini Phillip hakuwa amepanga kumwangusha mtoto ambae alimpa mafunzo mengi ya kijeshi na ya kisiasa. Inasemekena Alexander alirudi Macedoni baada ya miezi sita, kutokana na juhudi za rafiki wa familia, Demaratus, ambae aliongea na pande zote mbili.

Mwaka uliofuatia, gavana wa Persia aliyekuwa Caria, Pixodarus, alimtoa binti yake wa kwanza awe mke wa kaka wa Alexander kwa mama mwingine, Philp arrhidaeus. Olympias pamoja na watu wengine waliona jambo hili kama yalikuwa maandalizi ya kumfanya Arrhidaeus kuwa mfalme.

Alexander alikasirishwa na jambo hilo, alimtuma mwakilishi wake, Thessalus wa Corinth, kwenda kumbwambia Pixodarus kuwa, asimuozeshe mwanae kwa mtoto harumu, amuze yeye badala yake. Phillp aliposikia hayo, alisimamisha maandalizi ya harusi na alimkemea Alexander kuwa hakutaka amuoe mtoto wa Carian, kwakua alikua na binti bora zaidi kwa Alexander. Phillip aliwafukuza marafiki wanne wa Alexander, Harpalus, Nearchus, Ptolem na Erigyius, na aliwaamuru wa Corintho wamlete Thessalus akiwa amefungwa minyororo.

 

Ufalme wa Macedonia

 

Mauaji.

Alexander alitangazwa mfalme na wakuu wa serikali akiwa na umri wa miaka 20. Katika kiangazi cha mwaka 336 BC, wakati akiwa Aegae akihudhuria harusi ya binti yake aliyeitwa Cleopatra ambae ni dada wa baba mmoja mama mmoja na Alexander, aliyekuwa anaolewa na kaka yake Olypias, Alexander I wa Epirus, Phillip aliuwawa na captain wa mlinzi wake, Pausanias. Pausanias alijaribu kukimbia, lakini aliangukia dumu la mvinyo na aliuwawa na watu waliokuwa karibu wakiwemo marafiki wawili wa Alexander, Perdiccas na Leonnatus.

 

Kuunganisha nguvu za Utawala.

Alexander alianza ufalme wake kwa kwa kuwamaliza wahusika wote walioleta upingamizi kwenye taji lake. Alikuwa na binamu yake ambae alikuwa mwenye haki halisi ya kuwa mfalme wa Macedonia na alidhurumiwa haki ile na Philip. Alexander alimrisha auwawe. Pia watoto wa wafalme wa Lyncestis wauwawe lakini alimuacha mmoja Alexander Lyncestes. Olympias aliamuru Cleopatra Eurydice na Europa, ambae alikuwa ni binti aliyemzaa na Phillip, wauwawe kwa kuchomwa moto. Alexander aliposikia haya alikasika na alitoa amri Attalus auwawe, wakati huo Attlus alikuwa mjomba wa Cleopatra pia msimamizi wa Asia ndogo.

Attalus wakati huu alikuwa kwenye mawasiliano na Demosthenes, kuhusu uwezekano wa kuipiga Athens. Attalus pia alimtukana Alexander vibaya sana kwa kifo cha Cleopatra, Alexander aliona maisha ya Attalus ni hatari kwake, alimuacha Arrhidaeus ambae kwa wakati huu alikuwa taahira kabisa, inawezekana kwa sumu alizowekewa na Olympias.

 

Habari za kifo cha Philip zilisambaa kote na miji ilianza mapigano ikiwemo Thebes, Athens, Thessaly na Thracian ambayo ni makabila ya kaskazini mwa Macedon. Habari za mashambulizi hayo zilipomfikia Alexander, alijibu mashambulizi haraka. Ingawa alishauriwa atumie mbinu za ki diplomasia, Alexander aliongoza askari 3,000 wa Macedonia wenye farasi kuelekea kusini mpaka kufika Thessaly. Aliwakuta jeshi la Thessaly limechukua mlima Olympus na Mlima Ossa, na aliamuru wanajeshi wake waingilie Mlima Ossa. Watu wa Thessaly walipoamka asubuhi yake, walikuta Alexander amewazingira, waliamua kusarenda, alichukua farasi na magari yao na kuongeza kwenye jeshi lake. Aliendelea tena kusini mpaka kufikia Peloponness

Alexander alisimama thermopylae, ambako alitambuliwa kama kiongozi wa Amphictyonic League kabla ya kuelekea Corinth ambako ilikuwa kusini. Athens walitangaza amani kwa maandishi ya kisheria na Alexander alisamehe waasi. Mkutano mashuhuri uliojadiliwa sana katika historia uliotokea kati ya Alexander na Diogenes katika muda Alexander akiwa Corinth.

Wakati Alexander akimuuliza Diogenes anataka amfanyie nini, mwana philosopher kwa dharau alimwambia Alexander asogee kidogo kando kwani alizuia jua lisimfikie. Majibu haya yalimletea Alexander furaha ambae anaripotiwa kusema “Lakini kwa hakika, kama nisingekuwa Alexander, ningependa kuwa Diogenes.” Akiwa Corintho Alexander alichukua madaraka na alifanya kama Philip, aliwaandaa makamanda kwa vita vinavyokuja na Persia. Alipata pia taarifa ya mapigano yaliyoanza Thracia.

Mpango wa Balkan.

Kabla ya kuvuka kuelekea Asia, Alexander alitaka kuhakikisha usalama wa mipaka ya kaskazini. Miezi ya mwanzo ya 335 BC, alianzisha mashambulizi. Kuanzia mji wa Amphipolis, alisafiri mashariki kwenye nchi iliyokuwa huru ya Thracians; na Mlima Haemus, Jeshi la Macedona lilishambulia na kuyashinda majeshi ya Thracian. Jeshi hilo liliendelea kutembea kuelekea kwenye nchi ya Triballi, na kupumzisha majeshi kariby na mto Lyginus (kianzio cha mto Danube). Alexander baada ya hapo alitembea kwa siku tatu kuelekea Danube, alifanya mpango wa kuiingilia Getae kabila lililokuwa upande wa pili wa mto. Alivuka mto usiku, aliwashtua kwa majeshi yake kama cavalry skimish ulikuwa utaratibu wa majeshi ya enzi hizo.

Habari nyingine zilimfikia Alexander kuwa Cleitus, Mfalme wa Illyria, na Mfalme Glaukias wa Taulanti walianza mashambulizi ya kukaidi amri zake. Akitembeza jeshi lake kuelekea Illyria, Alexander aliwashinda wote na iliwabidi watawala wale wakimbie na majeshi yao. Kwa ushindi huu, Alexander alikuwa na uhakika na usalama wa upande wa kaskazini.

Wakati Alexander akikampan kaskazini, watu wa Thebans na Athens walianza upinzani wa wenyewe kwa wenyewe tena. Alexander kwa haraka alielekea kusini. Wakati miji mingine ikiwa na mashaka, Thebes uliamua kupigana. Theban walikuwa na mashambulizi makali na Alexander alishambulia mji na kuugawa utawala kati ya miji ya Boeotian. Mwisho wa Thebes uliiogopesha Athens na kuifanya Ugiriki itulie kwa muda. Alexander baadae aliamua kuanzisha kampaini ya Asia, akimuachia madaraka Antipater.

Ushindi wa Ufalme wa Persia.

Kilichoendelela yalikuwa mapigano ya Granicus, Utekaji wa Halicarnassaus na Utekaji wa Miletus

Ramani ya Ufalme wa Alexander na njia alizopitia.

Jeshi la Alexander lilivuka Hellespoint mwaka 334 BC likiwa na askari takriban 48,100, magari 6,100 ya farasi, meli 120 pamoja na mabaharia wapatao 38,000, waliotolewa kutoka Macedonia na miji mingine ya Kigiriki, askari wa kulipwa, na askari mateka kutoka Thrace, Paionia, na Illyria. (Hatahivyo, Arrian, ambae alimtumia Ptolemy kama chanzo cha habari anasema Alexander alivuka na farasi zaidi ya 5,000 na askari 30,000 wa miguu; Diodorus alinukuliwa akisema askari wengine waliopatikana kwenye rekodi ilikuwa; farasi 5,100 na askari 32,000 wa miguu. Diodorus pia anaelezea kulikuwa na majeshi mengine ambayo yalitangulizwa Asia ambayo Polyaenus katika maelezo yake ya katika Stratagems of War (5.44.4), alismea namba ya wanaume 10,000). Alisema alionyesha nia ya kuuteka ufalme wa Persia kwa kurusha upinde upande wa Asia na kusema anaikubali ardhi ya Asia kama zawadi kutoka kwa miungu. Pia Alexander alikuwa na eagle ya kupigana kuliko alivyokuwa baba yake, ambae alipendelea suluhu za kidiplomasia.

 

Baada ya ushindi wa kwanza dhidi ya majeshi ya Persia na Vita ya Granicus, Alexander alikubali Persia kuinua mikono kukubali kushindwa mji wa muhimu pamoja na vitu muhimu vya Sairdis; aliendelea tena kupitia pwani ya Ionian, aliipatia miji yake nguvu ya kujitawala yenyewe paia demokrasi. Miletus, ilishikiliwa na majeshi, ilihitaji utekaji wa mbinu kubwa pamoja na jeshi la majini la Persia yaliyokuwa karibu. Kuelekea Kusini Halicarnassus, katika Caria, Alexander alifanikiwa katika mipango yake ya utekaji mkubwa matokeo yake wapinzani wake, askari wa kukodiwa kapteni Memnon wa Rhodes pamoja na viongozi wa juu wa Persia na Caria akiwemo Orontobates, kuendelea mapambano ya baharini. Alexander aliacha serikali ya Caria chini ya ukoo wa Hecatomnid Ada ambae alimchukua Alexander kama mwanae.

Kifo cha Alexander.

Kati ya tarehe 10 au 11 June 323 BC, Alexander alikufa katika jumba la kifalme la Nebuchadenezzar II, mjini Babylon, akiwa na umri wa miaka 32. Kulikuwa na simulizi mbili juu ya kifo hicho, hata maelezo ya kifo yanatofautiana kidogo. Maelezo ya Plutarch ni kuwa takriban siku 14 kabla ya kifo chake, Alexander alimkaribisha afisa wa jeshi la majini Nearchus, alikaa nae usiku mzima na siku ya pili yake wakiwa wanakunywa pamoja na Medius wa Larissa (huyu alitoka familia katika familia mashuhuri na alikuwa rafiki wa Alexander). Baada ya hapo Alexander alipata homa iliyoendelea mpaka alishindwa kuongea. Askari wa chini, wakiwa na shauku juu ya afya yake, walipewa ruhusa ya kupita mbele yake huku akiwapungia mkono taratibu. Maelezo ya pili ni kutoka kwa Diodours ambayo yanasema Alexander alianza kusikia maumivu baada ya kunywa bakuli kubwa la mvinyo bila kuuchanganya, kwa heshima ya Heracles, hii ilifuatia siku 11 za ugonjwa na kupoteza nguvu, hakupata homa ila alikufa baada ya maumivu makali. Arrian pia anaelezea hadithi hii lakini Plutarch alikataa kabisa maelezo haya.

Kupitia madai ya watu wa hadhi ya juu wa Macedonia ni kuwa kifo cha Alexander kilisababishwa na mauaji. Kuanzia Diodorus, Plutarch, Arrian na Justin wote wanaelezea uwezekano wa kuwa Alexander aliwekewa sumu. Justin anaeleza kuwa Alexander alikuwa mhanga wa jaribio la sumu, Plutarch anapinga hili na kuwema ni uongo uliotengenezwa, wakati Diodorus na Arrian wote wanasema maelezo haya yamewekwa kama hitimisho la kifo. Maelezo yote haya ni kama yanakaribiana, na hivi karibuni Antipater (alikuwa generali wa Alexander) ameondolewa kwenye usemi kuwa alikuwa kiongozi wa mpango huo. Inawezekana baada ya maamuzi ya kifo chake kupelekwa Babylon, na kumuoana Parmenion na Philotas, Antipater ilivyovuma alipanga kifo cha Alexander kuwekewa sumu na mtoto wake Iollas ambae alikuwa mhudumu wa mvinyo wa Alexander. Kulikuwa pia na madai kuwa Aristotle alichangia.

Mabishano makali yaliendelea kuwa kama ilikuwa sumu isingeweza kuchukua siku 12 kumaliza maisha ya Alexander; wengine wanadai ilikuwa sumu iliyoua taratibu. Hata hivyo mwaka 2003 BBC walionyesha documentary iliyokuwa na uchunguzi wa kifo cha Alexander, Leo Schep kutoka New Zealand National Poisons Center alielezea mmea mweupe uitwao hellebore (Veratrum album), ambao ulijulikana kwa nyakati zile, inawezekana ulitumika kama kumuulia Alexander. Mwaka 2014 jarida la Clinical Toxicology Schep aliandika uwezekano wa mvinyo aliokunywa Alexander kuwe uliwekewa sumu ya Veratrum album, kwakuwa sumu hiyo inatoa dalili zote za kifo kinachoripotiwa juu ya Alexander katika kitabu cha “Alexander Romance”. Sumu ya Veratrum inatoa matokea taratibu na inawezekana kama Alexander aliwekewa sumu hiyo, inawezekana ikawa sababu kubwa ya kifo. Sababu nyingine kubwa ya kifo inayoelezewa mwaka 2010 ni kuwa, mazingira ya kifo chake yalitokana na maji ya mto Styx (mto Mavroneri wa leo), ambao inasemekana ulikuwa na sumu ya calicheamicin ambayo ni compound inayotoka kwenye bacteria.

 

Sababu nyingi zilizoweza kusababisha kifo cha Alexander zilielezewa, ikiwemo uwezekano wa kuugua malaria au typhoid. Mwaka 1998 chapisho la New England Journal of Medicine ilielezea kifo hicho kuwa kilisababishwa na homa ya typhoid na ilikuwa mbaya zaidi kwakuwa ililetea kuwa na vidonda kwenye utumbo na ilipelekea nerves za fahamu kupoteza nguvu. Uchunguzi mwingine wa hivi karibuni unaelezea pyogenic infection spondylities au meningitis. Wengine wanasema alipata maumivu makali ya wengu au West Nile virus. Maelezo mengine ni kuwa, afya ya Alexander inawezekana ilianza kudhoofika kwa muda mrefu baada ya miaka mingi ya kunywa mvinyo na pombe kali na pia vidonda na majeraha. Majonzi aliyoyapata baada ya kifo cha Hephaestion pia inawezekana yamechangia kifo chake.

Maisha binafsi ya Alexander.

Alexander alioa mara tatu: Roxana, mtoto wa Bactrian aliyetoka katika familia mashughuli ya Oxyartes, kutokana na mapenzi; na pia mtoto wa mfalme wa Persia princesses Stateira II na Parystatis II, mtoto wa Darius III na baadae mtoto wa Artaxerxes III, kwasababu za kisiasa. Alikuwa na watoto wakiume wawili Alexander IV wa Macedon wa Roxana na inawezekana Heracles wa Macedonia kutoka kwa hawara yake Barsine. Alifiwa na mtoto wa Roxana kwa miscarriage akiwa Babylon.

Alexander alikuwa na mahusiano ya karibu sana na rafiki ambae alikuwa bodyguard wake Hephaestion, mtoto aliyetoka katika familia mashughuli ya Macedonia. Kifo cha Hephaestion kilimpa Alexander majonzi makubwa. Hii pia inaelezewa ilichangia katika kudhoofika kwa afya ya Alexander ina inawezekana ilisababisha mental health state katika siku zake za mwisho.

Mahusiano ya kimapenzi ya Alexander ni kitu kitu kilichosababisha hisia na mabishano. Hakuna habari kamili katika historia inayoonyesha kuwa alijihusisha katika mapenzi ya jinsia moja au kuwa uhusiano wake na Hephaestion ulikuwa wa kimapenzi. Alelian, hatahivyo anaandika kuwa Alexander alitembelea Troy ambako aliweka maua kwenye makaburi ya Achilles na Hephaestion na kuwa Patroclus, katia barua kuna maelezo yanayoleta maana ya kuwa na maana kuwa mapenzi ya Hephaestion kwa Alexander yalikuwa sawa na mapenzi ya Patroclus kwa Achilles. Lakini neno eromenos (Kigiriki cha zamani) lilivyotumika hapa halina maana kuwa ni mahusiano ya kimapenzi. Lakini kuna uwezekano mkubwa kuwa Alexander alipenda kulala na wanawake na wanaume pia.

Green anabisha kuwa kuna ushahidi mdogo sana wa kuweza kusema Alexander alipenda mahusiano na wanawake; hakuzaa mrithi mpaka karibia siku za mwisho za maisha yake. Hata hivyo alikufa akiwa kijana sana, Ogden anasema mahusiano ya ndoa ya Alexander yanaridhisha kuliko ya baba yake akiwa katika umri wake. Mbali na wake zake, Alexander alikuwa na mahawara wengi.

Alexander alijipatia heshima ya wafalme wa Asia ya kuwa na wanawake wengi, lakini hakuitumia ipasavyo na alionyesha “self control” juu ya tamaa za mwili. Hata hivyo Plutarch alieleza jinsi Alexander alivyo ingiwa na moyo wa mapenzi kwa Roxana wakati akimsihi asimwingilie. Green anaongelea hili kama hiki ni kipindi Alexander alianza kuwa na hisia na mahusiano na wanawake akiwemo Ada wa Caria, ambae alimchukua kama mwanae, pia mama yake Darius Sisygambis, ambae inasemekana alikufa kwa majonzi baada ya kusikia kifo cha Alexander.


Kinglayz Wakuchana

378 Blog posts

Comments