BIASHARA 7 NZURI ZA KUFANYA ZITAKAZOKUINGIZIA PESA HATA KAMA UMELALA

Karibu kila mtu katika nyakati fulani hufikiria biashara za kufanya au njia za kutengeza pesa ambazo zitamletea pesa hata wakati wa usiku akiwa amelala. Hii maana yake ni kwamba biashara huingiza pesa hata kama mmiliki wa hiyo biashara hatakuwepo pale

BIASHARA 7 NZURI ZA KUFANYA ZITAKAZOKUINGIZIA PESA HATA KAMA UMELALA

 

Karibu kila mtu katika nyakati fulani hufikiria biashara za kufanya au njia za kutengeza pesa ambazo zitamletea pesa hata wakati wa usiku akiwa amelala. Hii maana yake ni kwamba biashara huingiza pesa hata kama mmiliki wa hiyo biashara hatakuwepo pale. Biashara nyingi humlipa yule mwenye biashara kulinganna na masaa anayotumia kuitumikia biashara husika. Unaweza kuona sasa kwamba biashara ya namna hiyo haina tofauti kubwa na ajira ya kawaida.

SOMA: Njia za kuingiza kipato nje ya  kazi yako.

 

Dhana hii ya kuingiza kipato ukiwa umelala inafanana sana au inakaribia kuwa sawa na dhana nyingine niliyowahi kuizungumzia katika kitabu nilichotunga kiitwacho MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA. Tofauti yake kubwa ni kwamba katika Mifereji ya pesa mtu unaweza kufanya biashara yeyote ile hata katika muda wako wa ziada itakayokupa kipato cha ziada wakati kuingiza pesa hata wakati  ukiwa umelala unatengeneza pesa kwa kutumia mfumo(AUTOMATION)

 

Kuna dhana iliyojengeka kwamba njia kubwa ya kuingiza pesa hata ukiwa umelala usiku wa manane ni kwa kupitia mtandao wa intaneti tu peke yake/biashara za mtandaoni au wengine mara nyingi huiita, njia ya kutengeneza pesa kupitia blogu. Lakini kiuhalisia mtu unaweza ukatengeneza pesa hata ukiwa umelala kwa kupitia biashara yeyote ile ilimradi tu umetengeneza mfumo(system) imara utakaowezesha shughuli kufanyika hata kama haupo pale. Hebu fikiria mmiliki wa mgahawa mkubwa wenye wafanyakazi kila idara kuanzia meneja mpaka mfagiaji, ana haja ya kuwa pale muda wote kweli?

SOMA: Biashara ya mgahawa wa chakula, mchanganuo na mtaji mdogo wa kuanzia.

 

Pamoja na kwamba kila biashara unaweza ukaitengenezea mazingira au mfumo wa kuiwezesha ikutiririshie noti hata ukiwa umelala usiku au ukiwa mapumziko wakati wa likizo, mapumziko wakati wa ujauzito, mapumziko baada ya kujifungua, mapumziko mwisho wa mwaka kama wenzangu kina Mangi wanapokwenda Moshi kuchinja ndafu wakati wa Krismasi nk. Huku nyuma ukiacha shughuli zako(biashara) zikiendelea kama kawaida na pesa ikiingia.

 

Haijalishi ukubwa wala udogo wa biashara, inaweza kuwa hata ni biashara ya mtaji wa laki moja, kinachozingatiwa hapa ni mfumo. Hata hivyo kumiliki biashara ya kukuingizia kipato hata ukiwa umelala siyo jambo rahisi sana lazima tuliweke wazi hili na nisingependa unafiki kuhubiri vitu visivyokuwa na uhalisia hapa ili kuwapa watu matumaini ‘feki’, kisa nisomwe na watu wengi.

 

Unatakiwa kufahamu ABC za biashara sawasawa kama  vile unavyoanzisha biashara yeyote ile nyingine, kuzingatia masuala nyeti kama vile suala la kufanya utafiti wa biashara husika pamoja na kuweka mpango wa biashara hiyo(mchanganuo), ni mambo ya msingi kabisa pamoja na kulijua soko lako vizuri.


Nirva_official

18 Blog posts

Comments