Nikajikuta kwa kweli nimekosea nikamwambia "samahani Angel sio vizuri ulichofanya ndio maana nimekua mkali japo sipendi kumfokea mwanamke". Akasema "usijali basi kama hapa ni kosa njoo huku" akanivuta kwa nguvu na kuniingiza chumbani kwake.
Ikumbukwe milango ilikua imefuatana hivyo ilikua rahisi sana kwake. Mle ndani Angel akafunga mlango na kuanza romance huku akiniramba masikio kwa kuingiza ulimi wake masikioni mwangu. Nilikua naenjoy sana yani.
Nikaona nijibu mashambulizi kama kawaida ya kaka yuu nikampa dawa kutwa mara tatu. Akaridhika nikaona nitoke zangu nikamwacha pale akiwa hoi bin taabani. Nikaingia ndani mwetu nilikokua na kaa na Jane huku nikijiuliza kazi ya Jane ni nini bila kupata majibu.
Nikakaa natafakari huku tv yetu ya mle ndani ikiwa iko on. Ghafla nikasikia "BREAKING NEWS" Maaskari sita wamekutwa wameuawa eneo la Usa river Arusha. Chanzo cha kifo chao ni kurushiana risasi na wanawake wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi. Majambazi hao walikua wametoka kutekeleza kifo cha mkuu wa mkoa wa Iringa aliyekua ziarani huko Arusha. Jitihada za kuwatia nguvuni zimegonga mwamba baada ya jeshi letu kuzidiwa nguvu na majambazi hao. Uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea na jeshi limeahidi kuwakamata mabinti hao". Ilikua mwisho wa ile taarifa.
Safari hii sikushtuka sana kwakua zile taarifa nilianza kuzizoea. Nikiwa nimeduwaa ghafla mlango ulisukumwa kwa nguvu akaingia Jane huku akihema sana. Kisha akasema yuu tafadhali kuna watu wanakuja humu ndani wapishe nusu saa tuu. Nikiwa sijamjibu niliona Jane anatiririka damu nyingi begani nilipomwuliza akanijibu kwa kuniambia naomba mkasi haraka.
Kwa kua alikua kaumia nikaona si vizuri kumjaza maswali. Nikaamua kumpa mkasi kama alivyoagiza. Akauchukua na kuutia sehemu ya jeraha huku akiwa ameumanisha meno nadhani ilikua ni kwa sababu ya maumivu. Kisha akavuta kwa nguvu kikadondoka kitu chini kikiwa na damdam nilikiangalia kwa makini na kugundua ni kipande cha risasi.
Nilishtuka sana kumwona Jane anajitoa risasi mwilini mwake. Nilitaka kumwuliza imekuaje nikashangaa mlango unagongwa na wakaingia wanawake wawili wakiwa wamevalia sare za jeshi. Nilijua wamekuja kumkamata Jane chaa ajabu wakampigia saluti na kuanza kumhudumia ile sehemu ya bega alipotolewa risasi. Nilibaki nashangaa pale kwani walikua wamejitosheleza kabisa kwa kila kitu.
Baada ya kumaliza waliaga wakaondoka zao. Jane alitoka kuwasindikiza mi nikabaki ndani huku kichwani mawazo mengi yakiwa yametawala nikijiuliza Jane ni nani. Akili ikanituma nichungulie nje kwa kua nlikua ghorofani hivyo mandhari ya nje ilionekana vizuri sana. Ambapo niliona kwa uzuri kabsa nje gari aina ya Landcruizer 110 ikiwa imenakishiwa kwa rangi ya kijani na madoamadoa meusi kama vile sare ya Jeshi. Kisha nikawaona wale wadada wakiingia humo na kumuaga Jane.
Nilikua nimeduwaa tu huku nikihisi ni ndoto ndefu sana ya usiku isiyoisha. Baada ya kumwona Jane anarudi nikaamua kukaa kitandani. Alipoingia "akanambia Yuu haya mambo unayoyaona humu yaishie humuhum". Mimi nikamwambia kwa sauti iliyokata tamaa ikichanganyikana na uoga "lakini Jane kwanini hutaki kuniweka wazi juu ya kazi yako maana sielewi". Leo nimeona wajeda wamekuja kukuhudumia, Umerudi umepigwa risasi begani hivi mi nitabaki gizani mpaka lini?"
Jane akageuka akanijibu" yuu nakupenda sana na sitaki kukupoteza nataka siku moja tuje tufunge ndoa japo maisha yangu huyaelewi. Lakini kama nilivyokwambia kua ipo siku nitakueleza A-Z juu yangu. Ila naomba kwa sasa uvumilie unayoyaona na uwe na kifua cha kutunza siri". Akazidi kusema kua na sababu ya kuja na wewe huku nilitaka ujue dunia kuliko uijuavyo. Hii dunia ina siri kubwa na ina mambo mengi kwani wewe ulijua mimi si mwanafunzi tu? Nikajibu ndio. Kisha akasema by the way kazi yangu imeisha leo ko tutaspend week moja af tutarudi Mbeya nikiwa nataka kujibu nilikatishwa na...