Mungu…. PEKE YAKE HAPATIKANI NA MAUTI." - I Timotheo 6:15,16.

Maandiko yanaeleza wazi kwamba katika maisha haya wanadamu wana hali ya kufa: yaani, wanakabiliwa na kifo. Lakini Yesu ajapo, mwili wetu utafanyiwa mabadiliko makubwa.

Sikilizeni, nawaambieni siri sisi hatutakufa sote, ila sote tutageuzwa, wakati wa mbiu ya mwisho, kwa nukta moja, kufumba na kufumbua. Maana tarumbeta ya mwisho itakapolia, wafu watafufuliwa katika hali ya kutokuweza kufa tena, na sisi tutageuzwa. Maana ni lazima kila kuharibikacho kijivalie hali ya kutoharibika, mwili uwezao kufa ujivalie hali ya kutokufa"- (1Wakorintho 15:51-53).

 

Sisi, kama wanadamu, hatuna miili isiyokufa sasa. Lakini ahadi inayotolewa kwa Mkristo ni kwamba sisi tutakuwa na miili isiyoweza kufa kamwe wakati Yesu atakapokuja tena kwa mara yake ya pili. Uhakika wa ahadi ya uzima wa milele ulionyeshwa wazi Yesu alipolipasua kaburi lake na:

"Lakini imefunuliwa kwetu sasa kwa kuja kwake Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Yeye amekomesha nguvu za kifo, na kwa njia ya Habari Njema akadhihirisha uhai usio na kifo" - 2Timotheo 1:10.

 

Mtazamo wa Mungu kuhusu mwisho wa wanadamu uko wazi: yaani, mauti ya milele kwa wale wanaomkataa Kristo na kuzing'ang'ania dhambi zao, au hali ya kutokufa kamwe kama zawadi kwa wale waliompokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wao wakati ule atakapokuja.

 

7. Kukikabili Kifo Cha Mpendwa Wetu

 

Hofu zile ambazo kwa kawaida sisi tunapambana nazo tunapokabiliana na kifo zinakuwa kali sana wakati ule anapokufa mpendwa wetu. Upweke pamoja na ile hisia ya kupotelewa, mambo hayo yanaweza kutulemea sana. Suluhisho pekee kwa utungu huo uliosababishwa na kutengana na mpendwa wetu ni ile faraja tu atupayo Kristo. Kumbuka kwamba huyo mpendwa wako amelala usingizi, na wapendwa wako wanaopumzika katika Kristo watafufuliwa katika ule "ufufuo wa uzima Yesu atakapokuja."

 

Mungu anapanga maajabu yake ya kuwaunganisha tena wale waliotengana. Watoto wadogo watarejeshwa kwa wazazi wao waliojaa furaha kubwa. Waume na wake zao watakumbatiana. Utengano wa kikatili uliotokea katika maisha haya utakwisha. "Mauti imemezwa kwa ushindi"- (1 Wakorintho 15:54).

 

Wengine wanajisikia vibaya sana kutengwa na mpendwa wao kiasi kwamba wanajaribu kufanya mawasiliano na wapendwa wao waliokufa kupitia kwa mjumbe wa mizimu (spiritualist medium) au kwa mtu yule anayeunganisha mawasiliano kama hayo wa Kizazi Kipya (New Age Channeler). Lakini Biblia kwa njia ya pekee inatuonya sisi dhidi ya kujaribu kupunguza maumivu yetu yanayotokana na kufiwa kwa njia hiyo:

"Baadhi watawaambieni "Nendeni mkatake shauri kwa mizimu na mizuka iliayo kama ndege; kwani ni kawaida watu kutaka shauri kwa miungu yao; na kutaka shauri kwa wafu kwa ajili ya walio hai" - (Isaya 8:19).

 

Ndiyo, Hivi kwa nini? Biblia inaeleza waziwazi kwamba wafu hawana fahamu yo yote. Suluhisho la kweli kwa huo uchungu uliosababishwa na kutengwa na mpendwa wetu ni ile faraja ambayo ni Kristo tu awezaye kutupa. Kutumia muda wetu kuwasiliana na Kristo ni njia bora kabisa kiafya ya kukua kupitia katika hatua hizo za kuhuzunisha.

 

Kumbuka siku zote kwamba, kule kuzipata fahamu tena kwa wale walalao katika Kristo kutawajia wakati ule zitakapopigwa kelele za kuja mara ya pili kwa Kristo ambazo zitawaamsha wafu!


Kinglayz Wakuchana

378 Blog posts

Comments