Forbes ilikadiria utajiri wa Kylie Jenner kukaribia dola bilioni 1
Forbes ilizua maoni mengi wakati ilisema kuwa nyota wa mitandao ya kijamii Kylie Jenner amepata utajiri wa karibu dola bilioni 1
Ni mafanikio ambayo watu wachache sana wanaweza kuyapata.
Kylie Jenner ajifungua mtoto wa kike
Kulikuwa na watu 5,700 kote duniani waliokuwa na utajiri unaozidi dola milioni 500 2017 kulingana na ripoti kutoka kwa Global Wealth Report.
Mabilionea halisi hata hivyo ni wachache. Lakini mtu anahitaji nini hadi kuitwa bilionea
1. Anzisha kampuni yako
Ukiangalia watu matajiri duniani kwa mfano Jeff Bezos wa Amazon, Mark Zuckerberg wa Facebook, Amancio Ortega wa Zara na Jack Ma wa Alibaba ndio wanatawala.
Forbes inawatambua watu thuluthi mbili ya mabilionea 2,208 kuwa waliojizolea utajiri wao na idadi hiyo inazidi kuongezeka.
Kylie Jenner kumshinda Mark Zuckerberg kwa kasi ya utajiri
Ni kweli kuwa neno utajiri wa kujizolea linaweza kuwa na ugumu kulielezea. Hatua ya Forbes kumtaja Kylie Jenner - ambaye alizaliwa katika familia tajiri kama aliyejipatia utajiri ilizua maoni mengi kwenye mtandao.
Jeff Bezos, chief executive officer of Amazon, arrives for the third day of the annual Allen Company Sun Valley Conference, July 13, 2017 in Sun Valley, Idaho.
Jeff Bezos, mwanzilishi wa Amazon, ndiye mtu tajiri zaidi dunaini
2. Kurithi pesa
Karibu thuluthi moja ya watu walio katika orodha ya Forbes walirithi pesa zao.
Hao ni pamoja na watu saba wa familia ya Walton, warithi wa maduka wa Walmart na Francoise Bettencourt-Meyers ambaye familia yake ilianzisha kampuni ya L'Oreal.
Mwanzilishi wa Amazon sasa ndiye mtu tajiri dunia
Urithi ni muhimu hasa barani Ulaya kutokana na kuwa umechangia kwa karibu nusu ya mabilionea kulinda na takwimu za Forbes za mwaka 2014.
Kuna sababu kadhaa zilizochangia watu ambao walirithi mali kuzidi kuongezeka.
Sababu moja ni kuwa thamani ya mali kama hisa imeongezeka kwa haraka kuliko mali nyingine miaka ya hivi karibuni.
3. Kuwa na mfuko wa uwekezaji
Kuna zaidi ya watu 140 katika sekta ya fedha walio na utajiri unaozidi dola blioni 2.5 kwenye orodha ya watu matajiri kwenye jarida la Forbes mwaka 2018.
Bill Gates achukua tena uongozi wa kuwa mtu tajiri duniani
Wengi wao ni kutoka nchini Marekani ambapo asilimia 25 ya mabilionea hupata utajiri wao kutoka sekta ya fedha.
Lakini usidhani kuwa ni rahisi kupata mafanikio hayo. Mkuu wa kampuni ya JP Morgan Chase boss Jamie Dimon ni baadhi ya mabilionea wachache waliochukua mkondo huo.
Abigail Johnson with Fidelity Investments
Abigail Johnson, ambaye anaismia mfuko wa uwekezaji wa babu yake wa Fidelity Investments, ni kati ya wanawake walio kwenye Forbes
Na wafadhili wengi karibu asilimia 20 ya watu matajiri zaidi ya 143 wana uhusiano na mifuko ya uwekezaji.
4.Hama Uingereza.
Idadi ya mabilionea nchini Uingereza ilishuka mwaka uliopita ambalo ni eneo tu duniani hali kama hiyo ilishuhudiwa kwa mujibu wa Forbes,
Eneo linaloshuhudia kuongezeka kwa watu matajiri duniani ni la Asia Pacific.
Karibu asilimia 29 ya watu mabilionea wapya mwaka uliopita walitokea eneo hilo kwa mujibu wa jarida la WealthX linalokadiria kuwa kuna mabilionea 2,750 duniani idadi iliyo juu kuliko ile ya Forbes.
Utajiri wa Aliko Dangote wapungua
China pekee ina mabilionea 29 kati ya 259 mabilionea wapya, idadi ya juu kuliko ua nchi yoyote.
Licha ya hatua zilizopigwa sehemu zingine duniani, Marekani inasalia nchi yenye mabilionea wengi zaidi ikiwa na mabilionea 585.
Alibaba founder Jack Ma
Mwanzilishi wa Alibaba Jack Ma ni mmoja wa watu maajiri zaidi nchini China
5. Usiwe na wasi wasi wa kufuata sheria
Mabilionea si wageni kwa kesi mahakamani. Kwa mfano Bill Gates, anawez kujulikana kama mtu tajiri wa kutoa misaada lakini historia yake si safi vile.
Mnamo miaka ya tisini Marekani iliishtaki kampuni ya Microsoft kwa kutumia mbinu zinazozuia ushindani.
Serikali ya Marekani ilishinda na Microsoft ikakata rufaa. Kesi hiyo iliishia makubaliano. Tume ya Ulaya nayo ishaipiga faini kampuni ya Microsoft.
Baddhi ya kampuni ambazo pia zimepigwa faini ni pamoja na Google na Samsung na piazile zisizo za teknolojia kama ya kamari ya Las Vegas Sands.