MAMBO 3 UNAYOTAKIWA KUYAACHA KAMA UNATAKA NDOA YAKO IDUMU

Hakuna ndoa yenye ukamilifu na isiyokuwa na changamoto. Wakati fulani yataibuka mambo kadhaa wa kadhaa, kwa sababu sisi ni binadamu. Hata hivyo, haimaanishi kuwa hatuwezi kufanya juhudi za kuwa na ndoa nzuri. Tunawezaje kuwa na ndoa nzuri?

 

MAMBO 3 UNAYOTAKIWA KUYAACHA KAMA UNATAKA NDOA YAKO IDUMU

Hakuna ndoa yenye ukamilifu na isiyokuwa na changamoto. Wakati fulani yataibuka mambo kadhaa wa kadhaa, kwa sababu sisi ni binadamu. Hata hivyo, haimaanishi kuwa hatuwezi kufanya juhudi za kuwa na ndoa nzuri. Tunawezaje  kuwa na ndoa nzuri? 

 

Tunaweza kuwa na ndoa nzuri kwa kuepuka kufanya vitu vinavyoifanya isiwe nzuri.

 

 Hapa, nimeweka mambo matatu, yafanyie kazi:

 

1. KUSHINDWA KUKUBALI KOSA

Kama wewe sio aina ya watu wanaokubali makosa pindi wanapokosea, basi ndoa yako itakumbwa na majaribu kayaya. Kusema “SAMAHANI” hakukufanyi kuwa dhaifu, bali hukufanya uonekane kuwa una ukomavu na uwajibikaji mkubwa wa kukubali kuwa umekosea na kwamba una utayari wa kurekebisha kosa husika. Mwenza wako anapolijua hilo, atakuwa tayari kukusamehe na kukupa nafasi nyingine, madamu samahani hiyo inatoka moyoni na ni ya ukweli.

 

2. KUMLINGANISHA MWENZA WAKO WA SASA NA YULE WA ZAMANI

Wakati fulani mtu hulifanya hili anapokuwa hafurahishwi na jambo lililofanywa na mwenza wake, lakini bado sio sahihi kufanya hivyo. Hutakiwi kumlinganisha mwenza wako na mpenzi wako wa zamani kwa hali yoyote ile. Huyo wa zamani ashakuwa wa zamani, anabaki kuwa ZILIPENDWA. Mwenza wako ni mwanadamu, hivyo anaweza kuhisi kuwa kwa kiasi fulani bado una mafungamano na mpenzi wako wa zamani pale unapoendelea kumzungumzia katika hali na mazingira hayo. Pia inaweza kumfanya ahisi kuwa hathaminiwi vya kutosha, hivyo usithubutu kufanya hivyo.

 

3. USIJARIBU KUBADILISHA SILIKA YA MWENZA WAKO

Kama unaingia kwenye uhusiano na mtu, jiandae kikamilifu. Mwanamke na mwanaume wanazo sifa za kiasili kabisa ambazo zinawatofautisha. Ni kama kusema mwanaume anatokea sayari ya Mars na mwanamke anatokea sayari ya Venus, hivyo ni viumbe wawili tofauti. Kama sifa za mwenza wako hazikuathiri moja kwa moja, usijaribu kuzibadilisha. Kujaribu kumbadilisha italeta picha kwamba humthamini vya kutosha, na unataka kumfanya awe mtu mwingine. Ila kama tabia zake zinampelekea kumuasi Allah, hapa itakuwa hakuna budi kumbadilisha tabia hizo kwa nasaa na njia tofauti tofauti.

 

 

EWE MOLA! ZIJAALIE NDOA ZETU ZIWE NA UCHAMUNGU NA UJIZAJE NA KILA LA KHERI NA BARAKA, NA UTUPE SUBRA YA KHALI YA JUU KATIKA IBADAH HII


Akili S Akili

191 Blog posts

Comments