Nilijihisi ufahamu nikiwa sehemu yenye majani mengi, giza likiwa limetanda na ukimya wa ajabu

Nilijihisi ufahamu nikiwa sehemu yenye majani mengi, giza likiwa limetanda na ukimya wa ajabu, sikusikia ndege wala Vyura wakilia kulitulia tuli, juu yangu niliona mbala mwezi ikiwa imefunikwa na mawingu lakini ikiangaza angani mwanga wake ulinipa taswira ya mahari nilipo, nilikuwa kwenye

Nilijihisi ufahamu nikiwa sehemu yenye majani mengi, giza likiwa limetanda na ukimya wa ajabu, sikusikia ndege wala Vyura wakilia kulitulia tuli, juu yangu niliona mbala mwezi ikiwa imefunikwa na mawingu lakini ikiangaza angani mwanga wake ulinipa taswira ya mahari nilipo, nilikuwa kwenye shimo huku nikiwa nimelala chali, sijui kilinipata nini nikawa pale, nikainuka haraka nikijishika mwili wangu kama nimeumia mahali, lakini nilikuwa salama salimini,juu palionekana ni mbali nikajua wazi nipo kwenye shimo refu sana. Mara nikasikia miungurumo kama ya radi, na wakati huu hali ya hewa nayo ikaanza badirika, hakikupita kitambo mvua ya ajabu ikaanza kunyesha, hali yangu ikaanza kuwa mbaya nikaanza kupapada nitafute kamba katika kuta za shimo lile sikuona kitu wala kushika kitu, mahali pengine nilishika miiba ikanichoma,sikujali nilikuwa katika hali ya kuokoa maisha yangu, nilijua maji yakijaa sitoweza salia katika ulimwengu huu,nikaanza jitihada za kupanda ukuta, mara ya kwanza nikatereza puu! Nikadondokea maji ambayo yalikuwa wameshaanza kutuama chini, nikajizoa zoa tena nikapanda mara ya pili wakati huu Nikishika maeneo ambayo nilihisi uwepo wa jiwe ama mti, nikaweza kupata kipande cha jiwe basi mbele yake nikiwa napapasa. Tena nishike chochote kwa juu nizidi jivuta juu, mara nikashika mwiba ukanichoma,kitu kama shoti kilisafiri mpaka kwenye ubongo wangu nikahisi maumivu na uchungu mkali kwenye ule mkono, hapo hapo sijakaa sawa nikateleza nilipokuwa nimekanyaga, puuh! Mpaka chini nikatota mwili wangu wote.

Nikasikia kwa mbali huko juu kama mtu alipita jirani na lile shimo, kulikuwa na mvua lakini nilizisikia vyema hatua za mtu yule, nikapaza sauti.

"Nakufaaaa, msaaadaa!"

Nikarudia kama mara tatu nikijizoa tena kuangalia juu, nikaona kivuli cha mtu akijongeaa kulikaribia shimo.

Kweli alikuwa mtu kavaa koti la mvua nilipomtazama sana nikahisi kumjua kwa sura, alifanana na kabisa na Sabrah.


Richard kibore

86 Blog posts

Comments