2 yrs - Translate

Aina 3 #Ushindi

Ambazo Yesu Alikuwa nazo #Yesu alishinda hivi vitatu, na ndio maana amekuwa mtangulizi aliyefanikiwa kwenye kila eneo.

Kama unataka kuwa mtu mkuu #Unataka kutumiwa na Mungu Kwa mambo makuuu ; unapaswa kuwa na hizi aina 3 za ushindi. Na hii ndio inaamua hatua ya MTU ya ukuaji wa kiroho.

#Soma kwa umakini wote

1. Ushindi dhidi ya #Ulimwengu !
[ Victory Over The World ]

Bwana Yesu Alisema haya maneno : #Yohana 16:33
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi #nimeushinda ulimwengu.

Tukisema ulimwengu maana yake ni MFUMO UNAOENDESHWA NA SHETANI, UNAOFANYA KAZI NA WANADAMU NA KUPITIA WANADAMU.

Kwa Mfano ; Kutajirika kwa kupitia Wizi, Rushwa, Utapeli, Uzinzi : Kwa Kifupi Ni #Kupata mafanikio ambayo yanamtoa Mungu na hayamuhusishi Mungu ( success that makes God be out of the equation ). Mafanikio yeyote iwe ni ndoa, Biashara, kazi, huduma ; Ukiona kwenye jambo Mungu hayupo UJUE UMEMEZWA NA #Ulimwengu.

Bwana Yesu alipitia Hii changamoto ; #Mathayo 4:8-9
[8]Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za #Ulimwengu, na fahari yake,
[9]akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.

Kama Mtoto wa Mungu unapaswa kuishi maisha yaliyo nje ya mfumo unaoendeshwa na Shetani

Tunakupa Kazi Lakini Uko Tayari Kufuta Ibada ya Jumapili
Ninakupa Kazi lakini uko tayari kulala na Mimi
Tunakupa Kazi lakini Uko tayari kuendana na masharti ya Miungu yetu
Tunakupa kazi lakini Uko tayari kuvaa tunavyotaka sisi Ili uvutie watu ?
Tunataka kukufanya maarufu ! Je uko tayari kufanya kama tunavyotaka.

HUU NDIO MFUMO WA ULIMWENGU
NI MFUMO WA SHETANI
( Ambao unakupa matokeo ya ChapChap Lakini yanagharimu nafsi Yako na roho yako ) shetani anaweza kukupa ulimwengu wote kwa siku Moja, lakini ni kwa gharama ya Roho yako. Shetani Hana shida na Fedha, ana shida na Roho yako.

Bwana Yesu Alisema Haya maneno
#Marko 8:36 Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?

UNASEMA NATAKA KUFANYA
MAMBO MAKUBWA NA MUNGU

1. Je umekuwa vya kutosha kuweza kuustahimili huu mfumo ( kusimama kinyume na huu mfumo )

2. Je Unafikiri moyoni mwako unachotaka ni Yesu au ni kwasababu hauna fedha. Kuna watu wanampenda Mungu ni kwasababu hawajasimama mbele ya fedha Fulani.

3. Je Una Nguvu za Mungu ndani yako kustahimili hii pressure ya Nje inayoletwa na ulimwengu.

Kuna Uhakika wa ushindi wa Moja Kwa Moja ; lakini una condition #Duniani mnayo Dhiki #Dhiki inayosemwa maana yake Kuna wakati , Utakaposema Mimi jumapili lazima niende ibadani, utaambiwa KAZI hauwezi kupata.

#Dhiki inayosemwa hapa maana yake Kuna wakati Utakosa Mchumba baada ya mchumba wako kukuambia Mimi sipendi mambo ya kanisa ( hata kama ana pesa nyingi kiasi Gani #Utawajibika kumwacha ), kama hauwezi maana yake ulimwengu unakuchukua.

Dhiki inayosemwa hapa maana yake Kuna wakati ; Utakosa Pesa Fulani ya haraka na ya Bure kwasababu ya aina Fulani ya masharti.

Dhiki inayosemwa hapa maana yake Kuna wakati Kuna wakati utakosa nafasi Fulani kwasababu #Ya maamuzi ya kuishika kweli.

#Yohana 16:33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi #nimeushinda ulimwengu.

Biblia inasema ; 1 #Yohana 5:4 Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.

IMANI YAKO ISIYO NA MASWALI #KWA MUNGU NA KWENYE NENO LAKE #NDIYO ITAKAYOKUPA USHINDI DHIDI YA ULIMWENGU.

Kama Bado uko nusu nusu ; Una maamuzi juu ya Neno la Mungu. Hautaweza kushinda.

NITAENDELEA WAKATI MWINGINE ; HIZO POINT 2 ZILIZOBAKI

Mungu akubariki

LivingWord|2023

Pastor Ibrahim Amasi

Install Palscity app