WEWE NI NANI MBELE ZA MUNGU NA WEWE NI NANI KWENYE MOYO WA MUNGU ITAAMUA KWELI KAMA SHIDA NI KILE UNACHOKIPITIA AU SHIDA NI WEWE TU.!!
Kwa sababu, wakati mwingne Shida inaweza isiwe kutaka kwenda Misri , Lakini shida ikawa unataka kwenda Misri Wewe ukiwa ni nani mbele za Mungu na Ukiwa nani kwa Mungu ; Maana hata Isaka alitaka sana kwenda Misri na bado Mungu akamzuia kuwa asijaribu kabisa kwenda Misri, maana kwake ilikuwa ni baraka Yeye kubaki Gerari kuliko kujaribu kwenda Misri. lakini kuna Mtu kama Yusufu, Yeye kwake kwenda Misri ni baraka mno kiasi kwamba hata kama Yeye kama Yeye hataki kwenda Misri lakini kwa vyovyote vile ni lazima atakwenda tu, na Mungu atalazimika kumpeleka huko huko Misri hata kama ni kwa kupitia njia ya kuuzwa na Kaka zake!
Ijulikane kuwa, Wengne wakijaribu kwenda Misri, basi huwa wanajikuta wameishia kuwa Watumwa tu huko. maana wapo wanaoenda Misri kwa sababu wana njaa na kwa sababu wanatafuta chakula ili kutibu njaa zao; Lakini kuna Yusufu ambae anaenda Misri kwa kuuzwa ili akawe Mtumwa na hatmae hawi mtumwa jumla na badala yake anaishia kuwa Makamu wa Rais. je' Wewe unataka kwenda Misri mwenyewe kwa sababu una njaa, au unaenda Misri kwa kuuzwa hata kama Wewe kama Wewe ulikuwa hautaki kwenda huko..?
kama Wewe ni Yusufu, basi usiogope kwenda Misri hata kama ni kwa kuuzwa kama mbuzi; Kwani kuuzwa sio shida, lakini cha muhimu ni kwamba huko Misri kuna u-Makamu wa Rais unakusubiria aiseee!
Wewe ni nani kwanza mbele.za Mungu na kwa Mungu, hii ni ya muhimu mno kabla ya kufika Misri au kabla ya kutaka kwenda Misri!
Wakati mwingne, Shida inaweza isiwe kutupiwa kwenye tanuru la moto, lakini shida ikawa ni unaenda kutupiwa kwenye tanuru la moto Wewe kama nani?
maana kuna Watu kama Meshaki, Shadraka na Abednego. Watu wenye majina ya hivi kwa vyovyote vile Mungu atahakikisha anawafanyia vitimbwi kupitia Mfalme Nebukadreza ili tu Siku moja watupiwe kwenye moto, tena moto wanaopaswa kutupiwa Watu wa hivi huwa ni lazima uchochewe mara7 zaidi.! (mpaka hapo shida sio kutupiwa kwenye tanuru la moto, lakini shida Wewe ni nani unayetakiwa kutupiwa kwenye tanuru la moto..?)
Na wakati mwingne, Shida inaweza isiwe kutupiwa kwenye zizi la simba wenye njaa kali, Lakini shida ikawa Wewe ni nani unayeenda kutupiwa kwenye zizi la simba; Kwani kuna Mtu kama Daniel, Yeye hata kama hataki kutupiwa humo kwa vyovyote vile ni lazima atatupiwa tu, na hata ikitokea akatupiwa katikati ya zizi la simba wenye njaa kali, heheeeeee! atakesha mkesha mzima na simba na kesho asubuhi ukienda kumsalimia utamkuta bado yumo yumo na hana kovu wala jeraha la jino wala kucha za simba katika mwili Wake!
Wewe ni nani mbele za Mungu ni kitu cha muhimu sana, ndio maana kuna kitu ambacho wengne wakikipitia huwa wanaishia hapo jumla; Lakini kuna wengne ikitokea wakapita hapo, basi ulimwengu lazima uandike habari zao na maisha yao hupandishwa jumla juu!
Pambana kwa vyovyote vile mpaka upate utambulisho wako mbele za Mungu na ifikie mahali Mungu mwenyewe awe ameushikilia utambulisho wako kwa namna ambayo hata ingetokea nini, basi Mungu ahakikishe hauangamii wala kupotea na badala yake Mungu ahakikishe kupitia kitu hicho unakuwa Mtu mkuu mno na ambae atakutukuza kwenye ukuu maradufu badala ya uhai wako kukatizwa!
Na wakati mwingne, kabla haujaanza kulalamikia unachokipitia au unayoyapitia, Nakusihi sana jiulize tu, hivi unayapitia hayo ukiwa Wewe ni nani mbele za Mungu na kwa Mungu; Kwani Wewe ni nani mbele za Mungu na Wewe ni nani kwenye moyo wa Mungu, hii ni muhimu mno kabla ya kuamua kulia au kulalamikia unachokipitia!
na wanaolia wote wakati wanapitia magumu kazini, kwenye masomo, ndoa, biashara, huduma n.k, hawa mara nyingi hawajui Wao ni akina nani mbele za Mungu wala kwenye moyo wa Mungu. kwani kuna Wengne kwenye moyo wa Mungu tumeshakuwa ni kama mboni ya jicho la Mungu kiasi kwamba hata ikitokea Tukafanyiwa hila na watu, basi Mungu mwenyewe atazigeuza hila hizo hizo kuwa baraka Kubwa mno kwetu!
(Mwanz45:4-1.
#Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja wampenda katika kuwapatia mema, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake jema.
(Rum8:28).
pamoja na yale unayoyapitia leo au yale yote utakayoyapitia huko mbeleni, lakini jiulize hivi Wewe ni nani mbele za Mungu na kwenye moyo wa Mungu Wewe ni nani..?
God bless You.
Mch.&Mwl. Dismas Herman
(Mwamsha Mashujaa, Waamsheni Mashujaa).
0752-878992.