2 yrs - Translate

#NI THURSDAY YA KUHESHIMIWA.Ni tarehe 25-8-2022.Leo ni siku ya 255 tokea tumeuanza mwaka huu wa 2022.Zimesalia siku 130 ilikutamatisha mwaka huu.Tunaendelea na wiki 35 ndani ya mwaka huu.Na
NenoLaLeo..MUNGU ATAKUHESHIMISHA HADHARANI.Matendo 16:35-40
Yule askari wa gereza alimpasha habari Paulo. "Mahakimu wametuma ujumbe ili mfunguliwe. Sasa mnaweza kutoka na kwenda zenu kwa amani."Lakini Paulo alimjibu,"Ati nini? Ingawa hatukuwa na kosa,walitupiga viboko hadharani hali sisi ni raia wa Roma.Tena, walitutia ndani na sasa wanataka kutufungulia kwa siri!Hata kidogo! Ni lazima wao wenyewe waje hapa watufungulie."Hao maofisa waliwapasha habari mahakimu juu ya jambo hilo,nao waliposikia kwamba Paulo na Sila walikuwa raia wa Roma, waliogopa.
Hivyo,walikwenda kuwataka radhi na baada ya kuwatoa ndani waliwaomba watoke katika mji ule.Muujiza wako hautakuwa Siri, lazima ijulikane kuwa Mungu ni mtetezi wako, ijulikane kwamba yuko upande wako na hashindwi,na yeye huheshimisha watoto wake.Pokea heshima kuu katika Jina la Yesu.Siku njema yenye kuheshimiwa pamoja na jamii yako.Tukutane Galilaya!...................

Install Palscity app