2 yrs - Translate

MKENYA HALISI

Mkenya mwenzangu,Sasa siasa zimebadilika nchini ,wananchi wanahitaji amani kando na mahitaji mengine ambayo serikali hukidhi.

Mungu ametupa nchi nzuri na yenye kupendeza ambapo Sisi ndio wamiliki na walinzi.

Twahitaji kusimama kidete na kupigania hadhi ya nchi yetu na tuweze kua kielelezo kwa Mataifa ya Afrika Mashariki na mataifa mengine.

Tarehe tisa mwezi huu,jummane ya wiki lijalo,wakenya tutajitokeza kupiga kura.Kila mmoja ana uhuru wa kumpigia kiongozi ampendaye.

Ninakuomba,piga kura yako ,umchague kiongozi aliye na mikakati mizuri kuelekea nchi yetu.

Sisi kama wenye nchi, tunahitaji biashara zetu ziimarishwe,Masomo,matibabu na nahitaji mengine yawe dhabiti, vijana wetu wapate kazi.Tuna mahitaji mengi sana.

Ili tufanikishe haya yote,twahitaji vitu vitatu:Umoja ,Amani na Upendo.Mpende mototo wako,mzazi wako,rafiki yako,jirani yako na yeyote utakayemuona katika maeneo yako.

Sisi wote ni wakenya na tunahitajiana katika ukuaji wa nchi,ninunue kwako nawe uniuzie ili tukuze nchi yetu, haswa kiuchumi.

Kumbuka kura huja na kupita,lakini mimi na wewe tunabaki, twawezaumia huku vijijini,kulingana na hali gumu ya maisha kama tu,tutafanya uamuzi mbaya .

Tufikirie kwa hayo.

Basi,nisaidie kufikisha ujumbe huu kwa jamii zetu vijijini kwa Kushare ujumbe huu.

Install Palscity app