Ukraine na Urusi zimesitisha mazungumzo ya kumaliza vita, wakati mzozo ukizuka kuhusu uwezekano wa kubadilishana wafungwa katika mji uliozingirwa wa Mariupol. Mjumbe mkuu wa Ukraine Mykhailo Podolyak amesema hatua zisingepigwa katika mazungumzo hayo kama Urusi haitaki kuitambua hali ilivyo kwenye uwanja wa mapambano.
Amesema madai ya Urusi kuwa inapambana na Unazi nchini Ukraine hayana msingi wowote. Ameongeza kuwa mpango wa kusitishwa mapigano unaweza kujadiliwa kama tu wanajeshi wa Urusi wataondoka nchini humo na maeneo yote yaliyokamatwa yakombolewe kikamilifu. Naibu waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi Andrei Rudenko alisema mazungumzo hayo hayatoendelea kwa sababu Ukraine imejiondoa.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alizungumza jana kwa njia ya simu na Rais Volodymyr Zelensky. Walikubaliana kuwa sululisho la mazungumzo ya kidiplomasia kati ya Ukraine na Urusi ni muhimu ili kumaliza vita hivyo.
SIBoman
Delete Comment
Are you sure that you want to delete this comment ?