3 yrs - Translate

Washikadau katika sekta ya utalii kaunti ya Lamu wametaja mila na tamaduni za wenyeji kuchangia katika ongezeko la idadi ya watalii wanaozuru eneo hilo.
Akizungumza na wanahabari kisiwani Amu, Mohammed Wenje msimamizi wa makavazi kisiwani humo ametaja hatua ya watalii, kutaka kufahamu kwa kina aina ya vyakula na maisha ya wanajamii hao, ikiwemo jinsi wanavyoadhimisha sherehe zao hasa za kitamaduni.
Aidha ametoa wito kwa wakazi kulinda tamaduni zao kwani ni njia mojawapo, itakayochangia katika kuimarika kwa sekta ya utalii kisiwani humo na hata kaunti ya Lamu kwa jumla.

image

Install Palscity app