4 yrs - Translate

#NenoLaLeo...
MKONO WA MUNGU UNA NGUVU! Yoshua 4:19-24
Waisraeli walivuka mto Yordani katika siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, wakapiga kambi huko mjini Gilgali, mashariki ya Yeriko. Yoshua akayasimika yale mawe kumi na mawili ambayo waliyachukua kutoka mtoni Yordani, huko Gilgali. Kisha Yoshua akawaambia Waisraeli, “Watoto wenu watakapowaulizeni siku zijazo, ‘Je, mawe haya yana maana gani?’ Mtawaambia hivi: ‘Taifa la Israeli lilivuka mto huu wa Yordani mahali pakavu.’ Mtawaambia kuwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliyakausha maji ya mto Yordani kwa ajili yenu mpaka mkavuka, kama alivyokausha bahari ya Shamu, kwa ajili yetu tukavuka, ili watu wote wa dunia wajue kuwa mkono wa Mwenyezi-Mungu una nguvu; nanyi mpate kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, milele.” Amina! Hakika mkono wa Bwana una nguvu, unatenda mambo ya ajabu na ukiwa juu yako utawashangaza wengi Naomba HUU MKONO UWE JUU YAKO, naijulikane ni Mkono uliojaa nguvu za kutisha!!Tukutane Galilaya! WEKESA

Install Palscity app