4 yrs - Translate

Wavuvi eneo la Watamu kaunti ya Kilifi wametakiwa na Mwenyekiti wa usimamizi wa bahari BMU eneo la Watamu Athman Mwambire kuchukua tahadhari wanapokuwa baharini.
Mwambire amesema bahari imekuwa ikichafuka mara kwa mara kutokana na mawimbi na upepo mkali ambao umekuwa ukishuhudiwa na kuhatarisha maisha na usalama wa wavuvi wanapoendeleza uvuvi wao kwenye bahari.
Akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu, amesema ipo haja ya wavuvi kujilinda na kuhakikisha usalama wao uko imara.
Aidha amewahimiza wavuvi ambao watavua kwa kipindi hiki kubeba vifaa vya kujisaidia endapo ajali itatokea na pia ametoa wito kwa serekali ya kauti na kitaifa kuwaletea vyombo zaidi vya uokozi ili ajali inapotokea msaada upatikane kwa haraka.

image

Install Palscity app