Unahofia kuaibika?
Unahofia kuumia?
Unahofia nini,?
Mara nyingi watu hatupend kukubaliana na hali halisi hata kama tumesha ujua UKWELI, lakin huendelea kutulia tukiamin kesho kutakuwa na mabadiliko.
Mfano
Umeambiwa unae mpenda ana mahusiano na watu wengine,lakin huachi ukijua eti kesho atatulia tu kwako.
Unapigwa,unatukanwa na kudharirishwa, kuna mda hadi simu unakatiwa au kuambiwa hakutak lakin bado unaamin kesho atakuwa mtu mzuri kwako.
Umempeleka mwanao shule za gharama toka cheke chea mpaka kidato cha 4,anafeli kwa kupata daraja la 4 afu unasema ana akili ila walim ndo wabovu..umesahau kuwa darasa lile lile wapo walio faulu zaid yake, hutak ukwel kuwa mwanao Mungu kamunyima akil ya darasan
We ni dada mrembo au kaka handsome na mwenye pesa,wakat watu wengine wanababaika na sifa zako lakin kuna mtu ambae kila ukikosea ana kuambia ukweli.
Kuna mtu ambae mulipendana ila alikuacha pamoja na pesa zako au urembo wako. Uliamin kuwa ana jeuri au kiburi kwa kuwa hukuwa tayar kuukubali ukweli kuwa sio kila mtu limbuken wa mwonekano wako au pesa zako.
Unaishi na siri moyon inayo endelea kukutesa. Unashindwa kuiweka wazi ukihis utaumbuka au utaachwa..kumbe kimya chako ndo aibu yako ya kesho.. Kuwa mkweli bora uchukiwe kwa kuwa mkweli kuliko kupendwa kwa uwongo.
Ukweli humuweka mtu huru
Hata kama yupo atakae umia kwa kuujua kweli ni bora zaid kuliko kukaa na uwongo huku nafsi yako iki kusuta