Hadi mwaka 1994 ilikuwa ikisadikika kuwa haiwezekani kuambukizwa UKIMWI zaidi ya mara moja, lakini baadae watu waligunduliwa waliokuwa na virusi vya UKIMWI vya zaidi ya kundi moja. Mwanzoni nadharia ya kuwa mtu wa aina hii alikuwa ameambukizwa virusi hao kwa mpigo kabla ya mwili wake kuweza kutoa kinga yake. Lakini sasa inafikiriwa kuwa maambukizi ya zaidi ya mara moja yanawezekana na hasa kama virusi hivyo ni vya makundi tofauti ingawa maelezo ya mazingira gani yanayoweza kusababisha hili kutokea hayajapatikana.
Aina Ya Virusi Na Tiba Zake
Dawa za kutibu UKIMWI – antiretroviral drugs (ARV)- wanaotokana na HIV-1, zilitengenezwa mahsusi kwa kutibu virusi wa kundi dogo B, haijathibitishwa kama dawa hii haifanyi vizuri kwa makundi mengine. Dawa zilizotengenenezwa kutibu virusi vya aina ya HIV-1 si zote zinazofanya kazi katika kutibu virusi vya HIV-2, kwa mfano, ARV inayoitwa NNRTI haifai tena kutibu virusi vy aina hii.
Ugumu wa kupata chanzo ya UKIMWI unatokana na uwepo wa aina mbalimbali za virusi na uwingi wa makundi madogo ya virusi hivi. Ugumu huo unachangiwa na kuwepo kwa aina tofauti ya makundi ya watu wanaotofautiana na wanaoupata ugonjwa huu kwa njia tofauti. Na hasa, ukweli kwamba mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa zaidi ya mara moja una maana kuwa kinga itakayotolewa kwa kundi moja la virusi haitafanya kazi kwa makundi mengine ya virusi.
VVU Walihamiaje Kwa Binadamu?
Ukweli kwamba virusi wanaweza kuhama kutoka aina moja ya mnyama hadi nyingine ulifahamika kwa miaka mingi sana na binadamu akiwa ni mnyama pia yupo kwenye hatari hiyo ya kupata maambukizi ya virusi kutoka kwa wanyama wengine. Tendo la kirusi kuhamia kutoka mnyama mwingine hadi kwa binadamu huitwa zoonosis.
Baadhi ya nadharia ya jinsi virusi hivi vilivyohamia kwa binadamu na jinsi SIV alivyogeuka na kuwa HIV ni hizi hapa:
Nadharia Ya Mwindaji – The ‘hunter’ theory: Nadharia hii ndiyo inayokubalika zaid kuliko nyingine. Nadharia hii inaseama kuwa virusi (SIVcpz) walihamia kwa binadamu kwa sababu sokwe waliuliwa na kuliwa au kwa sabau damu ya sikwe hao iliingia kwenye vidonda vya wawindaji hao.
chanzo cha UKIMWI
Nadharia Ya Kinga Ya Polio – The oral polio vaccine (OPV) theory:
Nadharia hii inasema kuwa chanzo cha UKIMWI kilianzia kwenye majaribio ya chanzo ya polio inayoitwa Chat iliyotolewa kwa watu karibu milioni moja wa Kongo, Ruanda na Burundi kwenye miaka ya 1950. Madai ni kuwa chanjo hiyo ilikuzwa ndani ya seli za figo za sokwe waliokuwa wana virusi wa SIVcmz na hivyo watu wengi
kuambukizwa na HIV-1.
Nadharia Ya Sindano – The contaminated needle theory: Hii ni mwendelezo wa nadharia ya mwindaji ambayo inasema kuwa pamoja na kuwa katika miaka ya mwanzo ya1950 sindano za kutumika mara moja zilikuwa zimeshaanza kutumika, katika nchi za Afrika wafanyakazi wa idara za afya waliendelea kutumia sindano moja kwa watu wengi kutokana na idadi kubwa ya sindano
iliyohitajika na gharama yake. Hii inaweza kuwa ilieneza virusi kotoka kwa mtu mmoja (kwa mfano mwindaji) hadi kwa mtu mwingine mwingine na kuruhusu virusi hao kujibadili kutoka aina moja hadi nyingine na kuzaliana.
Nadharia Ya Ukoloni – The colonialism theory: Nadharia ya ukoloni ni mpya na inaendeleza nadharia ya mwindaji na kuelezea ni vipi mambukizi ya mwanzo yaligeuka kuwa janga.
kuenea kwa ukimwi
Miaka ya mwisho ya karne ya 19 na ya mwanzo ya karne ya 20 yaliingiza Afrika kwenye ukoloni. Kwenye maeneo ya French Equatorial Africa na Belgian Congo, watawala hawakuwathamini watu waliowatawala na waafrika wengi wakajikuta kwenye makambi ambako hali za usafi zilikuwa duni, chakula kilikuwa kichache na matakwa kwa jumla yalikuwa mengi. Hali hii ilifanya afya ya watu hawa kuwa duni sana hivi kwamba virusi vya SIV viliweza kuwashambulia sana watu hawa. Kwa sababu ya afya yao mbovu, virusi hawa waliweza kubadilika na kuwa HIV. Sokwe aliyekuwa na virusi hivi alipokamatwa na kugeuzwa chakula, aliwaambukiza watu hawa.
Wafanyakazi hawa kwenye makambi walidungwa sindano anbazo hazikuchemshwa kuzuia magonjwa , kama ndui ili waendelee kufanya kazi na katika makambi mengi makahaba waliletwa kuwaburudisha. Watu wengi walikufa kwenye makambi haya hata kabla ya kuonyesha dalli za UKIMWI na huenda taarifa zilifichwa zilizoonyesha kuwa asilimia 50 ya wakazi walikufa kwenye makambi haya. Uwepo wa makambi haya unaendana kabisa na kipindi ambapo UKIMWI unasadidikika kuhamia kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu – miaka ya mwanzo ya karne ya 20.
Nadharia Ya Uangamizaji – The conspiracy theory: Nadharia nyingine inayoaminiwa ni ya uangamizaji au kuwa ni ugojnwa uliotengenezwa. Utafiti wa huko Marekani umeonyesha kuwa Wamarekani Weusi wanaamini kuwa VVU alitengenezwa kama vita ya kibaolojia iliyolenga kuangamiza kundi kubwa la watu weusi na mashoga. Wanaamini kuwa huu ulikuwa ni mpango uliofanywa na shirika la US Federal ‘Special Cancer Virus Program’ (SCVP) likisaidiwa na CIA. Inasadikika kuwa virusi hao walienezwa dunia nzima kwa makusudi au kwa bahati mbaya kupitia mpango wa
chanjo ya ndui au kupitia majaribio ya chanzo ya Hepatitis B kwa mashoga. Pamoja na kuwa nadharia kama hii haiwezi kupuuzwa, lakini moja kwa moja inaonekana kujengwa kwa kutumia fikra tu bila kujali mahusiano ya karibu ya SIV na HIV na kwamba UKIMWI umeonyesha kuwepo toka miaka ya 1959 | #Friend