Mara nyingine hutokea virusi vya aina mbili tofauti vikakutana katika seli moja ya mtu aliyeathirika na UKIMWI na kuzaa aina mpya ya kirusi, aina hizi huitwa CRFs “circulating recombinant forms” endapo virusi hivi vipya vitaonekana kwenye miili ya zaidi ya mtu mmoja. CRF A/B ni uzao wa virussi vya makundi madogo
ya A na B.
Aina Za Virusi Na CRFs Hupatikana Wapi?
Makundi haya madogo ya virusi vya UKIMWI vya aina ya HIV-1 na CRFs yamegawanyika kijiografia katika kuonekana kwake na kila eneo fulani la dunia lina kundi fulani lililostawi zaidi ya mengine. Makundi madogo ya HIV-1 yanayoonekana zaidi ni yale ya A na C. Utafiti unaonyesha kuwa sasa watu wanabainika kuwa na aina ya virusi ambavyo si vya asili ya eneo wanaloishi.
. Kundi dogo la A na CRF A/G huonekana zaidi Afrika Ya Kati na Afrika Magharibi. Kundi dogo la A ndilo linalosumbua nchi ya Urusi.
. Kundi dogo la B lina historia ya kupatikana bara la Ulaya, Marekani, Japan na Australia. Hili ni kundi linalopatikana hasa kwa wanaume wanaoshiriki ngono ya jinsia moja (mashoga).
. HIV-1 ya kundi dogo la C imeenea zaidi sehemu za Afrika Ya Kusini na Afrika Mashariki, India na Nepal. Hili ndilo kundi lililoleta madhara zaidi ya makundi mengine yote na nusu ya watu wote ambao wana UKIMWI wameathiriwa na kundi hili la kirusi.
UKIMWI barani Afrika
. Kundi la D hupatikana Afrika ya Kusini na Afrika Mashariki tu. CRF A/E kupatikana zaidi kusini mashariki mwa Asia lakini lilitokea Afrika ya Kati. Kundi dogo F limeonekana Afrika Ya Kati, Marekani Ya Kusini na Ulaya Ya Mashariki. Kundi G na CRF A/G yameonekana Afrika Magharibi na Afrika Mashariki na Ulaya Ya Kati.
. Kundi dogo H limeonekana Afrika Ya Kati, kundi dogo J Marekani ya Kati na K hupatikana Kongo (DRC) na Kameruni tu.
Mategemeo ni kuwa makundi madogo ya UKIMWI na CRFs yatazidi kupatikana kutokana na kuwa makundi huzaliwa pale kirusi wa kundi moja anapokutana na kirusi wa kundi jingine na makundi haya yaliyopo yatazidi kuenea na kuonekana maeneo mengine ambako sasa hivi hayajaonekana.
Kuna Uhusiano Wa Aina Ya Kirusi Na Kupata UKIMWI?
Utafiti mmoja uliofanyika nchini Uganda mnamo 2006 ulionyesha kuwa watu walioambulizwa virusi vya UKIMWI vya kundi dogo D au/na CRFs zake walipata UKIMWI mapema zaidi kuliko wale wa kundi dogo A na walikufa mapema zaidi kama hawakupewa tiba ya ARV. Watafiti hao wakashuri kuwa kundi dogo hili la D ni hatari
zaidi kwa kuwa linajishika zaidi kwenye seli za kinga za mwili. Ufafiti unaofanana na huo ulifanyika pia nchini Kenya mwaka 2007 kwa wanawake wenye virusi hao wa kundi dogo D na kuonyesha kuwa walikuwa kwenye hatari ya kufa zaidi ya wale waliokuwa na kundi dogo A. Utafiti mwingine nchini nchini Senegali (1999) ulionyesha kuwa wanawake wengi zaidi walioathirika na makundi madogo C, D na G walipata UKIMWI katika miaka miatano baada ya maambukizi mapema zaidi kuliko wale wa kundi dogo A.
Utafiti mwingine nchini Thailand ulionyesha kuwa watu wailokuwa na virusi vya kundi dogo CRF A/F walipata UKIMWI na kufa mapema zaidi kuliko wale wa Kundi dogo B, kama hawakupata tiba ya ARV.
Katika kurasa nyingine utaweza kusoma jinsi virusi vya UKIMWI vilivyohamia kwa binadamu kutoka kwa wanyama na kuelezea ugonjwa wa UKIMWI, dalii zake na tiba inayotumika hadi sasa. Kuna mada nyingine pia kuhusu ugonjwa wa mlipuko wa Corona (COVID-19.)
Tunakuomba ndugu msomaji utoe maoni yako kuhusu mada yetu hii ya leo na usisite vilevile kuuliza maswali uliyo nayo. Tutafurahi sana kushirikiana na wewe.
Kwa maelezo zaidi na ya kina, tuma ujumbe kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapo chini, au tutumie barua pepe kupitia promota927.com au tupigie simu kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu | #Friend