Seif Yusuph created a new article
3 yrs - Translate

Katika mfululizo wa mada hii, nitajaribu kuonyesha ni nini wataalamu mbalimbali wanasema kuhusu ugonjwa wa UKIMWI – tutaona virusi Vya UKIMWI ni nini na nadharia zinazotolewa kuhusu chanzo cha UKIMWI na baadaye kujadili kuhusu dalili za ugonjwa huu, jinsi unavyofanya maambukizi na mwisho jinsi ya kuutibu
ugonjwa wa UKIMWI.Chanzo cha UKIMWI na VVU ni kitu ambacho kimeendelea kuwaduwaza wanasayansi tangu ugonjwa huo ulipoanza
kujulikana kwenye miaka ya 1980. Kipindi chote toka muda huo, somo hili limekuwa chanzo cha mijadala mikali na nadharia nyingi zimekuwa zikitolewa, kama za mpango wa siri wa chanjo. Ukweli wa suala hili uko wapi? Na ugonjwa huu wa UKIMWI ulitoka wapi haswa?Ugonjwa huu ulibainika kwa mara ya kwanza kabisa nchini Marekani mwazoni mwa miaka ya 1980. Baadhi ya mashoga (wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja) huko New York na california walianza kuonyesha ghafla maambukizi na kansa ambazo hazikukubali tiba ya aina yo yote. Wakati huo, jina la UKIMWI
halikuwepo, lakini ilionekana dhahiri kuwa watu hawa walikuwa wanaugua maradhi yaliyofanana.

Ugunduzi wa Virusi vya UKIMWI ulifuatia mara moja. Ingawa kuna baadhi ya watu wanakataa kabisa hadi leo kuvihusisha virusi hivyo na ugonjwa wa UKIMWI, ushahidi ni wa kutosha kabisa kwamba UKIMWI hutokana na Virusi vya UKIMWI (VVU). Kwa hiyo basi, tukitaka kujua UKIMWI umetoka wapi inatubidi kufahamu kwanza
chanzo cha VVU. Ni vipi, lini na wapi virusi hivi vilianza kuleta ugonjwa kwa binadamu.



Virusi Vya UKIMWI (VVU)



Virusi vya UKIMWI ni vya aina ya virusi wanaochukua muda mrefu sana kuleta madhara kwenye mwili baada ya maambukizi (lentivirus), ambao wanashambulia mfumo wa kinga za mwili. Virusi vya aina hii vimeonekana kwenye wanyama wengi wakiwemo paka, kondoo, punda na ng’ombe. Kwa mafaa ya mada yetu ya kutafiti chanzo cha VvU, lentivirus ambaye ni kivitio ni Simian Immunodeficiency Virus (SIV) ambaye hushambulia nyani,
kirusi anayeaminika kuwa na umri wa karibu miaka 32,000.

Inaaminika kuwa VVU ni uzao wa SIV kwa sababu baadhi ya vizazi vya SIV vina tabia za karibu sana na HIV-1 na HIV-2 ambazo ni aina mbili za VVU. HIV-2, kwa mfano, wanafanana sana na S/Vsm ambao ni kizazi cha SIV kilichoonekana kwenye aina ya nyani anayepatikana Afrika Magharibi aitwaye Sooty mangabey au
White-collared monkey. Na aina ya VVU inayosumbua sana na kuambukiza sana, HIV-1 imeonekana kuwa na tabia za S/Vcpz ambaye ni SIV anayepatikana kwa sokwe.



ukimwi toka kwa nyani

white-collared mangabey



Mnamo Februari 1999 kikundi cha wanasayansi wa Marekani, baada ya utafiti wa miaka 10 mfululizo kuhusu chanzo cha UKIMWI, walitangaza kuwa waligundua aina ya kirusi wa SIVcpz ambaye alifanana sana na HIV-1. Kirusi huyu aligundulika kutoka aina moja ya sokwe wa Afrika Magharibi na moja kwa moja wakatangaza kuwa
sokwe ndiye chanzo cha kirusi wa UKIMWI cha aina ya HIV-1 na kwamba kirusi huyu aliambukizwa kutoka kwa sokwe hadi kwa binadamu. Wakatoa machapisho kuwa sokwe pori waliambukizwa na aina mbili tofauti za virusi (simian immunodeficiency viruses) kwa wakati mmmoja na katika kujamiiana, alipatikana kirusi wa
aina ya tatu ambaye alienezwa kwa sokwe wengine na hatimaye kwa binadamu na kusababisha UKIMWI.Walieleza pia kuwa makundi yote ya HIV-1 – yaani kundi M, N na O – yaliyotokana na sokwe hawa na kila kundi liliambukizwa kwa binadamu kwa wakati tofauti.
Virusi Vya UKIMWI Vya HIV-1 Na HIV-2.

Virusi vya ukimwi vipo vya aina nyingi sana na vinabadilika haraka sana. Hii ina maana kuwa kuna mikondo mingi ya vizazi vya virusi hata ndani ya mwili mmoja wa mtu aliyeathirika na UKIMWI. Kulingana na tabia za kiurithi, virusi vinaweza kugawanywa kwa aina, makundi na makundi madogo.

Kuna aina mbili za virusi vya UKUMWI: HIV-1 na HIV-2. Aina zote mbili husambazwa kwa ngono, kupitia damu na kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Aina hizi mbili huleta madhara yanayofanana lakini HIV-2 haviambukizwi kiurahisi kama HIV-1 na muda kati ya kuambukizwa HIV-2 na kuugua ni mrefu zaidi. Katika dunia watu wengi zaidi huambukizwa HIV-1 na mtu akitamka VVU bila kufafanua, huwa ana maana ya HIV-1. HIV-2 wapo zaidi Afrika Magharibu na hupatikana kwa nadra sehemu nyingine.



Virusi Vya HIV-1


Mikondo ya uzazi wa HIV-1 inaweza kugawanywa katika makundi manne: Kundi kuu M, kundi O na makundi mapya ya N na P. Makundi haya yanaweza kuonyesha namna nne ya jinsi SIV alivyohamia kwa binadamu. Kundi O hupatikana Afrika Magharibu Ya Kati tu na kundi N lililogundulika mwaka 1998 huko Kameruni hupatikana kwa nadra sana. Kundi P lilipatikana kwa mwanamke wa Kameruni mwka 2009. Zaidi ya asilimia 90 ya maabukizi ya HIV-1 ni ya kundi M. Chini ya kundi hili la M, kuna makundi madogo kama tisa yenye utofauti kidogo kitabia, nayo yameitwa A,B,C,D.F,G,H,J,K na CRFs. | #Friend

Katika mfululizo wa mada hii, nitajaribu kuonyesha ni nini wataalamu mbalimbali wanasema kuhusu ugonjwa wa UKIMWI – tuta

Katika mfululizo wa mada hii, nitajaribu kuonyesha ni nini wataalamu mbalimbali wanasema kuhusu ugonjwa wa UKIMWI – tuta

Katika mfululizo wa mada hii, nitajaribu kuonyesha ni nini wataalamu mbalimbali wanasema kuhusu ugonjwa wa UKIMWI – tutaona virusi Vya UKIMWI ni nini na nadharia zinazotolewa kuhusu chanzo cha UKIMWI na baadaye kujadili kuhusu dalili za ugonjwa huu, jinsi unavyofanya maambukizi na mwisho

Install Palscity app