alijiandaa na kwenda kwenye shughuli zake, kisha Sophia nae akaamka na kujiandaa kisha akelekea kwakina Jane kwani alishajipanga kutimiza anachokitaka kwa siku hiyo.
Kama alivyoambiwa na Yule mganga yani alipokaribia tu kwakina Jane akatafuna kile kijani kisha akafika na kumuulizia Jane ambapo walienda kumuitia, Jane alitoka na kushangaa aliyemfata pale kwao kisha akamsikiliza lengo lake ambapo Sophia alimwambia kuwa anamuomba nyumbani kwake. Jane alitaka kukataa ila akakumbuka maneno ya Ibra kuwa yeye ndio faraja ya huyu Sophy mke wa Ibra kwahiyo Jane akakubali na kumwambia kuwa akioga tu ataenda.
Akaagana nae pale, kisha Sophia akawa anarudi nyumbani kwake huku akifurahia kuhusu Yule mganga kuwa ni kiboko kwani hakutegemea kama Jane angekubsali kirahisi namna ile.
Sophia alipofika tu kwake, akachukua ile dawa na kuinyunyuzia mlangoni kisha akaenda jikoni na kuweka juisi kwenye glasi kisha kuweka na ile dawa ili Jane akija tu ampe juisi hiyo.
Muda kidogo Jane nae aliwasili ambapo cha kwanza kabisa alipofika mlangoni alishangaa kuona kama unga unga na kumuuliza Sophia,
“Dada ni nini hiki mlangoni?”
“Wewe pita tu kuna vitu vilianguka”
KwakweliSophia hakupendezwa kabisa na hili swali la Jane kwani alizidi kujidhihirisha kuwa ni mchawi, Jane aliingia ndani na kukaa pale sebleni kisha Sophia akaenda jikoni kumletea ile juisi.
Wakati Sophia akitoka jikoni na ile juisi akamshangaa Jane akiwa ametulia kabisa akiangalia Tv ambayo yeye hakuiwasha | #All