Ukiona una mume au mke ambaye kila mkitofautiana unakujakusikia maneno kutoka kwa wazazi au nduguzake unajua fika kuwa aliwaambia au kwenda kukushtakia kwao basi fahamu kabisa kwamba umeoana na mtoto mchanga mwenye umbo la mtu mzima, bado kuna vitu vya muhimu kuhusu ndoa alikuwa hajavifahamu, tafuta namna ya kuongea naye au ikiwa ngumu sana tafuta ushauri kwa mwenye hekima na aliyepevuka kuliko yeye ili amsaidie maana ndani ya huyo mwenza wako bado kuna akili za kucheza mdako na kombolela na anahitaji kuifahamu ndoa kabla hajaifanya kuwa doa