2 yrs - Translate

Pichani, mtoto wa Nyani akiwa ameng’ang’ania kwenye maiti ya mama yake iliyoko mdomoni mwa Simba. Japokuwa mwili wa mamaye hauna uhai, lakini mtoto wa Nyani bado anaamini kumkumbatia mamaye ni salama zaidi kuliko kujaribu kukimbia.

Bado anamwamini mama yake!! Wazungu wanasema “Down With The Ship”. Maana yake, umeamua kufia ndani ya meli inayozama. Au umeamua kuzama nayo!

Hebu angalia macho ya mtoto na alivyong’ang’ania mwili wa mamaye.
Bado anaamini mama atatafuta namna ya kumwokoa, kumbe mama hayupo tena.

Kuning’inia kwenye tumbo la mamaye ndiyo usalama wa hali ya juu anaoujua tangu azaliwe. Mara zote wakati mama anaruka kwenye matawi ya miti mikubwa yeye huwa amejishika tumboni kwa mama. Ana imani sana na sehemu hiyo.Ndiyo maana ameamua kwenda “Down With The Ship.”

Kuna kubwa la kujifunza kwenye hili tukio. Nimewaza mengi wakati natafakari hii picha, hasa kwa vile nina watoto wanaonipenda na kunitegemea.

Kama wazazi tujue kuwa watoto wetu wanatutegemea kwa kiwango ambacho maisha yao yanategemea yetu. Baya lolote kwetu, kifo chetu, kuugua kwetu kunayaathiri maisha yao moja kwa moja.

Leo hii unadharau familia yako na kuwajali ZAIDI rafiki zako wa kazini, kwenye vilabu vya pombe na sehemu nyingine za starehe. Familia yako unaipa muda kidogo sana na wala huoni umuhimu mkubwa wa kuwa na familia yako. Mambo mengi unawaza na kuamua KIBINAFSI SANA. Unataka kujifurahisha wewe kwa starehe za muda zisizo salama bila kujali athari zinazoweza kuipata familia kwa maamuzi yako!

Kumbuka, baya lolote kwako litaathiri wanao moja kwa moja. Rafiki na wengine wana maisha yao nje ya wewe, lakini kwa wanao wewe ndiyo kila kitu, kama unavyomwona mtoto wa Nyani kwenye hii picha, mama yake ndiyo kila kitu. Watoto wako wanaweza kuendelea kuishi bila wewe ila maisha yao yatakuwa yameharibika kabisa. Wao ndiyo watakaoipata “Down With The Ship.”

Tafadhali, ukishakuwa na familia, weka mbele familia yako. Maslahi yao iwe kipaumbele cha kwanza kwako. Wasije wakazama na wewe kwenye majanga unayovuna kwa kuendekeza UBINAFSI na starehe zisizo salama.

Ni kweli, wakati mwingine mambo mabaya hutokea tu na hayakwepeki, lakini ni wajibu wetu kujilinda na kumwomba Mungu atulinde.

Be careful. Wajibika. Jizuie linda familia yako.

Ubarikiwe sana🙏🏾🙏🏾

image

Install Palscity app