3 yrs - Translate

MATANGAZO

Ferdinand Omanyala: Kwanini mtu mwenye kasi zaidi Afrika hakukatishwa tamaa na marufuku aliyowekewa?
By Celestine Karoney
BBC Sport Africa, Nairobi
21 Septemba 2021, 085 EAT
Kenya's Ferdinand Omurwa Omanyala (left) breaking the African 100m record finishing behind Trayvon Bromell (centre) but ahead of Justin GatlinCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Licha ya kuwa wa pili baada ya Trayvon Bromell, mwanariadha wa Kenya Omanyala aliweka rekodi ya mbio za mita 100 Jumamosi

Ferdinand Omurwa Omanyala anaweza kuwa ndiye mwanaume mwenye kasi zaidi barani Afrika baada ya kuvunja rekodi ya bara la Afrika katika mbio za mita 100, lakini Mkenya huyo anakiri kuwa marufuku ya matumizi ya dawa za kututumua misuli michezoni aliyowekewa mwaka 2017 itaathiri mafanikio yake.

Alikimbia kwa kasi ya sekunde 9.77 katika mbio za Kip Keino Classic mjini Nairobi na kuvunja rekodi ya sekunde 9.85 iliyowekwa na raia wa Afrika Kusini Akani Simbine mwezi Julai.

"Wakati wote ninapokimbia mbio hizi za kasi, watu huzungumza, lakini kwangu mimi ni kwa ajili yangu- Sikimbii kwa ajili ya mtu mwingine ," Aliiambia BBC Afrika michezo, kijana huyu mwenye umri wa miaka 25.

Muda wake unamfanya kuwa mwanaume wa nane mwenye kasi zaidi kuwahi kushuhudiwa, licha ya kumaliza mbio akiwa wa pili akimfuata Mmarekani Trayvon Bromell ambaye pia aliweka rekodi bora binafsi ya sekunde 9.76.

Omanyala ambaye alianza kazi yake ya riadha katika mwaka 2016, aliwekewa marufuku ya miezi 14 mwaka 2017 , baada ya vipimo kuonyesha kuwa alikuwa ametumia dawa za kututumua misuli michezoni, ambazo binafsi anasema zilikuwa ni dawa za kuondoa maumivu alizokuwa amemeza.

"Nilihisi nilikuwa muathiriwa wa hali," alieleza. "Ilikuwa ni dawa ya kumaliza maumivu halafu ikageuka kuwa ilikuwa na steroid ndani, na masaibu hayo yamenifanya kuwa mtu niliye sasa ."

"Ilinipa uvumilivu, ikanifanya kuwa imara -kwasababu ni changamoto ambayo hakuna mwanariadha ambaye angependa kuipitia- na ni funzo kwamba hupaswi kutumia kitu chochote na haupaswi kumuamini mtu yeyote katika riadha."

"Imekuwa vigumu lakini ilinifanya niache yaliyopita nyuma. Tunasamehe, tunasahau na kusonga mbele. Mimi ni yule mtu ambaye anaishi maisha ya wakati huo. Imekuwa safari ngumu kuanzia mwaka 2016-majeraha, marufuku-lakini yote hayo ni mambo yaliyopita. Tunaandaa hali ya baadaye ."

'Hakuna ukomo katika uwezekano'

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Ferdinand Omurwa Omanyala aliweka rekodi ya kitaifa nchini Kenya mara mbili kwa kushinda mita 100 katika Tokyo Olympiki

Omanyala anasisitiza kuwa anaweza kukimbia kwa kasi hata zaidi na ameweka rekodi ya chini ya sekunde 9.70 kama lengo lake, mafanikio ambayo yamefikiwa tu na magwiji kama vile Usain Bolt wa Jamaica, na Yohan Blake na Mmarekani Tyson Gay.

Mchezaji huyo wa zamani wa raga aliyegeuka na kuwa mkimbiaji wa mbio za kazi za masafa mafupi-anaamini kuwa anaweza kukimbia hata kwa kasi kubwa zaidi kuliko hiyo, na labda kukaribia rekodi ya dunia ya Bolt ya sekunde 9.58.

"Hakuna ukomo katika uwezekano ," alitabasamu.

Msimu huu umekuwa wa mafanikio kwani ameweza kufuzu kwa michuano ya robo fainali katika mbio za mita 100 katika Olympiki za kwanza, huku akiweka rekodi mpya ya Kenya ya sekunde 10.00 , akiwa ni mmoja kati ya watu watano waliofanikiwa zaidi katika kipindi cha miezi saba iliyopita.

"Nimekuwa nikipata mafanikio katika kila mbio kwasababu nimekuwa nikikimbia katika mashindano mengi sana mwaka huu ," anasema. "Hilo ndilo nitakalolifanya mwaka ujao na nitaanza mapema labda mwezi Machi . Kwahiyo itakapofika Juni, tutegemee mida ya kasi sana ."

Matumaini ya kuhamasisha
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Mwanariadha wa mbio fupi Mmarekani Justin Gatlin ana matumaini kwamba Afrika inaweza kutoa wanariadha wenye kasi zaidi duniani siku zijazo

Katika nchi inayofahamika kwa kuwa na wanariadha bora katika mbio za masafa ya kati na masafa marefu, Omanyala sasa analenga kuhamasisha kizazi kijacho cha wanariadha wa masafa mafupi Wakenya.

"Ombi langu kubwa ni kwamba katika miaka mitano ijayo tuwe na akina Omanyala, watoto zaidi wanaoweza kukimbia mbio za masafa mafupi, kwasababu mimi ni wa kwanza ambaye nilijaribu kung'ang'ana kufika juu ,"anasema.

"Ninafahamu kuna watu wengi ambao wanaweza kukimbia kwa kasi, katika soka na raga, kwahiyo kama tutaweza kuwapata wakimbiaji wa mbio fupi 10, Kenya itakuwa imepata mafanikio.

"Sasa wanaamini inawezekana , kwasababu wengi wa watu waliokuwa wakiingia katika mbio hizi walikuwa wanakatishwa tamaa na wazazi wao au watu wengine wakisema 'huwezi kufika popote nchini Kenya kwa mbio za masafa mafupi'. Lakini sasa watu wanaamini hii inawezekana.

"Sasa ninataka kufungua klabu ya mbio za kasi za masafa mafupi na kuwatia moyo wakimbiaji vijana kufanya mazoezi na kuona ni wapi wanaweza kwenda."

Mwanaume mmoja anayeamini kwamba Omanyala, Simbine na Mnigeria kama Enoch Adegoke, aliyefikia finali ya Olympiki mita 100 watawatia moyo Waafrika wenzao ni Mshindi wa zamani wa Olympiki na dunia Justin Gatlin.

Mmarekani huyo, aliyemaliza nyuma kidogo ya Omanyala Jumamosi pia alielezea mafanikio ya Waafrka matika matukio ya viwanjani.

"Kipaji cha mbio za masafa mafupi za kazi katika Afrika ni kikubwa," aliimbia BBC.

"Dunia hinawaona wanariadha wa Afrika kama wakimbiaji wa mbio za masafa marefu tu , lakini sasa kuna warusha tufe, warukaji , wakimbiaji wa mbio za kasi za masafa mafupi , kwahiyo ninadhani imeonyesha duniakwamba inazaidi kuliko kipaji cha masafa marefu tu.

"Hicho ni kitu kikubwa kuwa nacho.Nimekuwa kila mara nikiamini kwamba Afrika ina mengi ya kutoa kwa dunia zaidi ya kile ilicho nacho tayari."

Wanaume wenye kasi zaidi katika historia:

Usain Bolt (Jamaica) - sekunde 9.58
Tyson Gay (Marekani) - sekunde9.69
Yohan Blake (Jamaica) - sekunde 9.69
Asafa Powell (Jamaica) - sekunde 9.72
Justin Gatlin (Marekani) - sekunde 9.74
Christian Coleman (Marekani) - sekunde 9.76
Trayvon Bromell (Marekani) - sekunde 9.76
Ferdinand Omanyala (Kenya) - Sekunde 9.77s
Nesta Carter (Jamaica) - sekunde 9.78
Maurice Greene (Marekani ) - sekunde 9.79
Mada zinazohusiana
Michezo
Kenya
Riadha
Habari kuu
Moja kwa mojaPaul Rusesabagina: Mzozo wa kidiplomasia waibuka baina ya Rwanda na Ubelgiji
Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 21.09.2021
Saa 3 zilizopita
'Siwezi kuacha muziki hata kama Taliban hawakubali'
Saa 3 zilizopita
Gumzo mitandaoni
Je! ni vijidudu gani tunasambaziana wakati tunabusu?
20 Septemba 2021
Viumbe sita wenye uwezo wa kuishi kwa maelfu ya miaka kabla ya kufa
20 Septemba 2021
Akutana na mama yake kwa mara ya kwanza baada ya miaka 58
21 Septemba 2021
Mwanariadha mwenye kasi zaidi Afrika hakukatishwa tamaa na marufuku ya dawa
21 Septemba 2021
Je Paul Rusesabagina ni nani?
20 Septemba 2021
Zifahamu taaluma sita ambazo zinatokomea
18 Septemba 2021
Teksi zageuka kuwa shamba la mboga Thailand
20 Septemba 2021
Hali ikoje kujifungua chini ya utawala wa Taliban?
20 Septemba 2021
9:36
Video,Ndoto za mitaaniensi ndio maisha yangu, Muda 9,36
20 Septemba 2021
Iliyosomwa zaidi
1
Usiyoyajua kuhusu ibada za waabudu shetani
2
Viumbe sita wenye uwezo wa kuishi kwa maelfu ya miaka kabla ya kufa
3
Makubaliano AUKUS: Je ni kwanini manowari za nyuklia zinaogopwa kote duniani?
4
Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 21.09.2021

image

Install Palscity app