3 yrs - Translate

Kwenye Maisha kuna wakati huwa unaitwa “Breaking Point”.

Kwa Mujibu wa Mwandishi maarufu wa vitabu Lisa Gupta, anasema kuwa *“ Everyone has a breaking Point, No matter, how strong they are” _Akimaanisha bila kujali una Nguvu/Uhodari wa kiasi gani lazima utapitia wakati huu._

Huu Ni wakati ambao unaona Nguvu zimekuishia na hakuna tumaini tena,

Una maumivu makali ya Ndani na hauoni sababu ya kuishi tena,

Unatafakari na unaona uwekezaji na nguvu zote ulizoweka kwa Miaka mingi zinapotea bure,

Unaona Giza na hauoni namna unaweza kutoka, ni Kama umebaki peke yako,

Una madeni yanakuandama na yamekupa stress kiwango cha Juu,

Kuna kitu kimetokea na kimekupa aibu hautamani sura yako ionekane tena, unatamani kupotea usionekane.

Mtu wako wa Ndani AMEUMIA na AMEJERUHIKA, unahisi KUCHOKA.

Kila SHUJAA LAZIMA APITIE hali hii kabla hajaitwa shujaa.

Ufanye nini: Make Your Breaking Point To Be Your Turning Point. Ukiona hali hii ujue unaingia MSIMU MPYA wa MAISHA YAKO.

Usikate tamaa bado kuna Tumaini, angalia SOMO kubwa unalolipata na baada ya hapa usirudie Makosa tena.

Nakuombea WIKI HII, MUNGU AKUVUSHE KWENYE CHANGAMOTO INAYOKUKABILI.

*_#MrLegendary_* ✍🏽✍🏽✍🏽✍🏽

Install Palscity app