*TUNZA SHATI LANGU USILICHAFUE.*
Watu wawili walikuwa wanakunywa pombe baa.
Wakati wanakunywa wakaanza kubishana na baadaye ule ubishi ukawa ugomvi.
Mmoja akamrukia mwenzake akaanza kumpiga.
Baada ya kumpiga kwa muda mrefu akagundua kuwa mwenzake hapumui tena.
Kumbe amemwua mwenzie.
Ndipo alipoanza kukimbia huku shati lake likiwa limechafuka sana na damu.
Wale waliyokuwa wanauangalia ule ugomvi wakaanza kumfukuza.
Huyu mwuaji akakimbilia kwenye nyumba ya mtu mmoja mcha Mungu na akamwomba yule mtu amfiche maana ameua mtu na watu walikuwa wanamfukuza.
Yule mcha Mungu akasema nitakuficha wapi wakati mimi nina chumba kimoja tu?
Yule mwuaji akamjibu akamwambia acha kuendelea kupoteza wakati fikiria tu mahali pa kunificha.
Yule mcha Mungu akavua shati lake safi akampa yule mwuaji alafu yeye akachukua lile shati la muaji lililojaa damu akalivaa.
Akampa sharti yule mwuaji na kumwambia tunza shati langu usilichafue.
Yule mcha Mungu alipofungua mlango wa chumba chake wale watu wakamvamia na kumpiga sana wakijua yeye ndo mwuaji huku mwuaji akiondoka salama na kurudi kwake.
Baada ya kumpiga sana yule ndugu akapelekwa polisi na baadaye akapelekwa mahakamani na akahukumiwa kunyongwa kwa kumwua mtu mwingine.
Yule mwuaji halisi akiwa kule nyumbani alijisikia vibaya sana akaenda mahakamani akajisalimisha akasema yeye ndiye aliyeua, yule ndugu aachiwe huru.
Hakimu akamwambia umechelewa, yule ndugu kesha nyongwa.
Alilia sana na kujiambia kuwa yule mtu amekufa kwa kosa ambalo sio lake.
Akakumbuka maneno ya mwisho ya yule ndugu *"LITUNZE SHATI LANGU USILICHAFUE."*
Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zako na zangu.
Alichukua vazi letu lililochafuliwa na uchafu wa dhambi zetu akatupa vazi Lake takatifu la haki.
Yesu aliuawa kwa kosa lako na langu.
Akatupa haki Yake na kutuambia tusichafue tena maisha yetu.
Kuendelea kutenda dhambi baada ya yale ambayo Yesu ametufanyia ni kuidharau sana kazi ya msalaba na kuikanyagia chini Damu Yake ambayo tumesafishwa kwayo.
Ni kushindwa kuthamini kuwa kuna mtu alishakufa kwa ajili yetu.
Ni kushindwa kutambua uthamani wa wokovu ambao tumeupokea.
Tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu namna hii.
*LITUNZE SHATI LANGU USILICHAFUE.*
Collin Njoroge
Delete Comment
Are you sure that you want to delete this comment ?
Ntwarabakiga Innocent
Delete Comment
Are you sure that you want to delete this comment ?