3 yrs - Translate

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 20.08.2021: Lingard, Salah, Diallo, Lewandowski, Tchouameni, Nunez, Sarr
Dakika 39 zilizopita
Kiungo wa kati wa England Jesse Lingard, 28
Maelezo ya picha,
Kiungo wa kati wa England Jesse Lingard, 28

Kiungo wa kati wa England Jesse Lingard, 28, yuko tayari kuondoka Manchester United kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa pengine tu iwe anaamini atacheza mara kwa mara kwa timu ya Ole Gunnar Solskjaer msimu huu. (Times - subscription required)

Mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski yuko tayari kwa changamoto mpya mbali na Bayern Munich. Mchezaji huyo wa miaka 32 bado amesalia na miaka miwili kumaliza mkataba wake na mabingwa wa Bundesliga. (Mirror)

Chelsea imeripotiwa kufanya mazungumzo mapya na kiungo wa kati wa Monaco Aurelien Tchouameni. Mfaransa huyo wa miaka 21 pia amehusishwa na Manchester United katika chote cha msimu. (Simon Phillips, via Express)

Mohamed Salah
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Mohamed Salah

Liverpool wanaandaa ofa mpya ya mkataba kwa mshambuliaji wa Misri, Mohamed Salah, 29, ambayo itakuwa ghali zaidi katika historia ya kilabu. (Athletic - subscription required)

Pierre-Emerick Aubameyang anafurahi kusalia Arsenal hata baada ya kipindi cha uhamisho. Barcelona ilisemekana kuwa na nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Gabon lakini mchezaji huyo wa miaka 32 anataka kutimiza lengo lake la kuwa gwiji wa Gunners. (Express)

Brighton wapo kwenye mazungumzo na Benfica juu ya uhamisho wa pauni milioni 25 kwa mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, 22. (Mail)

Amad Diallo
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Sheffield United inavutiwa kumsajili winga wa Manchester United na Ivory Coast, Amad Diallo, 19, kwa mkopo. (Sky Sports)

Hornets wameripotiwa kumruhusu mmoja wa wachezaji wao aondoke wakati ambapo mshambuliaji wa Nigeria Isaac Success, 25, anapaswa kufanya uchunguzi wa matibabu na Udinese ya Italia. (Gianluca di Marzio)

Rais wa Fiorentina Rocco Commisso anasisitiza kuwa hajaweka bei ya kumuulizia mlengwa wake anayechezea Manchester City na Tottenham, Dusan Vlahovic. Mshambuliaji huyo wa Serbia mwenye umri wa miaka 21 tayari amevutia dau la euro milioni 70 kutoka kwa mabingwa wa Uhispania Atletico Madrid. (TGR Rai Toscana, via Inside Futbol)

Watford inataka pauni milioni 36 kwa ajili ya mshambuliaji Ismaila Sarr
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Watford hawajapata yeyote anayemwinda winga wa Senegal Ismaila Sarr, 23, msimu huu na amesalia kuwa mchezaji imara - ambaye amehusishwa na kuhamia Liverpool - lakini hauzwi. (Watford Observer)

Kocha wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino anasema mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, ni "mtulivu" tu licha ya uvumi mpya unaomhusisha na kuhamia Real Madrid. (Metro)

Southampton inafikiria kumchukua beki wa Everton, Thierry Small. Kijana huyo wa miaka 17 amehusishwa na kuondoka Goodison Park wakati kuna ripoti kwamba amekataa kutia saini mkataba mpya na Toffees. (Hampshire Live)

Barcelona wanataka pauni milioni 12.8 kwa kiungo wa kati wa Uhispania Ilaix Moriba. Kijana huyo ananyatiwa na Wolves lakini kilabu cha Kikatalani bado hakijapokea ofa inayokubalika. (ARA via Molineux News)

Samuel Umtiti
CHANZO CHA PICHA,AFP
Maelezo ya picha,
Samuel Umtiti mchezaji wa Barcelona

Everton imewasiliana na Barcelona kumchunguza beki wa kati Samuel Umtiti, 27, kwa nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kabla ya tarehe ya mwisho ya uhamisho mnamo Agosti 31. (Express, via Goodison News)

Manchester United wameonekana nchini Ureno wakiangalia ushindi wa mchujo wa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa wa Benfica dhidi ya PSV Eindhoven huko Estadio da Luz. (A Bola - in Portuguese)

Install Palscity app