3 yrs - Translate

MPIGA PICHA

NA GREYSON H MTINGWA

WHATSAPP. 0742893359.

SEHEMU YA KWANZA.


Mara ya kwanza kukutana nae alinivutia sana. Siwezi kumsahau maana nilitokea kumpenda. Ni mzuri anavutia. Anasifa ya kuwa mke, na kwa mwonekano wa nje amekamilika kila idala.
Mweupe mwenye asili ya kiarabu. Nywere ndefu za shombe shombe. Pua ndefu, mrefu na si mfupi kwa kimo. Saizi ya kati na si mnene wala mwembamba kwa umbo. Kifuani alikuwa kajaa na kufanya avutie maana viembe dodo viliishika vizuri t-shet yake ya rangi nyeupe aliyokuwa amevaa. Katikati alikuwa katenganishwa vizuri na kufanya muunganiko wa umbo namba nane. Hakika alikuwa na umbo namba nane. Nyonga iliyokuwa imetanuka kwa ustadi mkubwa ilikuwa imehifaziwa ndani ya suruali nyeusi ya njinsi fulani hivi laini. Alipendeza mara dufu baada ya kutabasamu. Nilipatwa na kigugumizi kumsemesha, lakini aliponifikia alinisalimu. Sauti yake ilivutia na kufurahisha ngoma za masikio yangu. Kigugumizi kilinipata kujibu salamu yake. Japo kwa shida niliitikia salamu yake. Nilisimama pembeni nimwache apite ili nimwone kwa nyuma. Waaaaooo alikuwa kabeba mzigo wa maana. Kila alipopiga hatua nyuma kulitingishika. Haswaa..... alikuwa anapendeza kumtazama. Hakika Muumba hakukosea kuumba alimuumba haswa. Acha nimwite african beauty japo sio yule wa diamond.
Hivyo ndivyo alivyo kuwa kwa nje.

***************

Usiku ulifika nilifunga ofisi yangu na kuanza safari ya kurejea nyumbani. Kutoka mahari nilipokuwa nafanyia kazi mpaka kufika nyumbani kwetu ilikuwa ni mwendo wa kama nusu saa hivi. Kwa umri wangu wa miaka 23 nilikuwa bado naishi nyumbani kwa wazazi wangu. Sikuwa nimeanza kujitegemea, na si kwamba sikuwa naweza kujitegemea. Hapana ni wazazi tu ndio walitaka niwe nyumbani mpaka mda umri ule....

Familia yetu ilikuwa ni familia ya kidini tena yenye imani haswa. Katika familia yetu tulizaliwa watoto watatu. Wa kiume wawili na wakike mmoja. Mimi kama first born. Nilipewa heshima sana nyumbani nilikuwa na uhuru wa kusikilizwa. Wa pili alikuwa mdogo wangu wakike Alice. Wa mwisho alikuwa Misago. Alice alikuwa akisoma kidato cha tano katika shule ya sekondari Ifunda girls. Huku Misago ambaye alitumia jina la babu mzaa mama alikuwa akisoma darasa la tano katika shule ya msingi ya private nje na mkoa wa Mwanza.

Baada ya kumaliza chuo kikuu na kukaa mtaani kwa mda mrefu bila kuajiriwa. Nilielekeza lawama zangu kwa wazazi hasa baba mzee Damian. Baba yangu mzee Damian ni mwalimu wa shule ya sekondari Mwenge, kwa sasa amebakiza miaka miwili astafu kazi. Mama yangu Caroline yeye ni nesi katika hospital ya wilaya Nyamagana. Baba alipenda sana mimi nisomee ualimu, japo kwa upande wangu mimi nilikuwa napenda sana kusomea mambo ya uandishi wa habari na utangazaji. Nilibadili mawazo yangu na ndoto zangu za kuja kuwa mwandishi mkubwa ama mtangazaji wa television mkubwa. Nilijikuta nikiangukia kusomea maswala ya ualimu tena ualimu wa masomo ya historia na geografia.

Mwaka mmoja baada ya kumaliza elimu yangu ya chuo kikuu kupitia kozi ya ualimu. Sikuweza kupata ajira. Mwaka na sehemu ulipita nikiwa mtaani bila ajira yeyote. Baada ya mda kupita na kuona mambo ya kusubili kuajiriwa sio sawa. Niliamua kuwekeza na kufungua ofisi yangu ambayo ilikuwa inajihusisha na k upigaji wa picha na kusafisha. Mwanzo ulikuwa mgumu lakini sikukata tamaa. Nilikuwa nikipiga picha kwenye sherehe za kipaimara, sendoff, ndoa kichenpart, graduation na pia kwenye happy birthday na pia kwenye shuguri zingine nyingi.

Taratibu nilianza kujulikana na kuwa maarufu. Na jina langu kukua. Nilikuwa nafanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo yangu. Pesa nilikuwa napata za kutosha kuweza kuishi mwenyewe lakini nguvu ya wazazi ilinifanya nifate watakavyo wao.

Hatimae, miezi ilikatika nikawa si mtu yule wa kukaa mtaani na kulalamikia serikali kuhusu ajira. Sikuwa nasubili tena ajira kutoka serikalini, bali nilikuwa nimetoa ajira kwa vijana wanne ambao niliwafundisha kazi. Vijana walikuwa wakijituma haswa.

*******************

Baada ya kufunga ofisi niliwakabizi vijana wangu wa kazi ujila wao wa siku, kisha mimi nikaanza safari ya kuelekea nyumbani. Sikiwa na appointment na mtu yeyote hivyo sikuwa na sehemu yeyote ya kupita, moja kwa moja nilielekea nyumbani. Nilipofika nyumbani kitu cha kwanza nilielekea bafuni kuoga. Baada ya kuoga nilibadili nguo na kwenda kuungana na familia kwa ajiri ya chakula cha usiku.

"Lukas naona mambo sio mabaya mwanangu." Aliongea baba baada ya kumaliza kula chakula.

"Hapana baba kawaida tu kwani vipi?" Nilimjibu baba.

"Sikusikii tena ukilalamika kuhusu serikali kutoa ajira........ maana kipindi cha nyuma nilikuwa nakusikia kila mara ukitupia lawama serikali." Baba aliendelea kuonge.

"Akili ilikuwa bado haijakoma tu baba lakini sasa sina tatizo kabsa." Niliongea.

"Ndio kusema kwamba hata zikitoka ajira huwezi kwenda mwanangu." Aliongea mama aliekuwa amekaa pembeni kwa baba.

"Yani mama kwa kipato nachokipata kwa sasa hata sina shida tena ya hizo ajira. Akiri yangu saizi inawaza mambo makubwa ambayo nauhakika kama nikisubili kuajiriwa sitaweza kuyatimiza." Niliongea kwa kujiamini.

Baada ya maongezi tulitawanyika kila mmoja na kwenda kulala.

Asubuhi ya siku iliyofata niliamka mapema kama kawaida yangu. Nilijianda kisha nikaelekea mezani kupata kifungua kinywa. Ilikuwa kawaida kwetu kila siku ifikapo saa moja lazima chai iwepo mezani. Nilikunywa chai na siresi tatu za mkate kisha nikatoka na kuanza safari ya kuelekea ofisini kwangu. Nilipofika ofisini niliwakuta vijana tiali washa fika. Kama kawaida niligawaia majukumu ya kazi kila mmoja nilimpa kadi ya mwaliko wa kwenda kupiga picha kutoka katika sherehe nilizokuwa nimepata kadi.

Siku ilienda poa sana jioni vijana walirudi na picha. Siku zote kitu ukikifanyia ubunifu lazima kitapendwa na wengi. Ndivyo ilivyo kuwa hata kwenye kazi yangu. Baada ya vijana wangu wa kazi kuwasirisha kazi nilizichukua na kuziweka kwenye laptop yangu na kuanza kuziwekea mandhari nzuri ili kuzipendezesha zaidi. Kwa kutumia faili la adobe photo shop nilikuwa nikizitengeneza picha na kuzifanya ziwe na mwonekano angavu.

"Tino hii picha vipi mpaka hapa unaionaje si iko poa sana." Nilimuliza kijana wangu mmoja wa kazi ambae alikuwa akinifatilia kipindi nikiwa naifanyia editing ile picha.

"Hapa boss mbona mwake picha imetoka unaweza sema location ilikuwa UK vile." Aliongea Tino.


****ITAENDELEA *********

image

Install Palscity app