Je Wajua Kuhusu Ufugaji Wa Mende Na Faida Zake?


Kwa kawaida tumezoea kuua wadudu wanao ruka na wanao tambaa kwa dawa zenye sum kali kwao na kuwateketeza kabisa, Ni sawa kwani upande mwingine nivyema kufanya au kuweka mazingira yawe safi katika maeneo tunayo ishi, Miongoni mwa wadudu hao tunao waua kila siku ni pamoja na mdudu MENDE ambaye leo nataka nikueleze kua unaweza kujitengenezea kipato kwa kutumia mdudu mende.
Katika jamii yetu ya kitanzania watu wanaweza kukushangaa na kukuona pengine wewe ni kichaa eidha unaamini katika ushirikina kwa kukuona umeamua wewe kwa hiari yako kuga MENDE.
Leo tuzungumzie kuhusu faida za kufuga MENDE
Ufugaji wa mende unalipa sana kwani niufagaji ambao hauna ghrarama sana na wenye soko kubwa kwani katika nchi kama China, Autralia na Denmak chakula kikuu cha mifugo yao hasa kuku ni mende.
Kama ulikua hujui ni kwamba Kilomoja ya mende kwa matumizi ya Chakula cha kuku inauzwa 50,000TSH mpaka 70,000TSH na kwa matumizi ya binadam inauzwa 85,000TSH mpaka 100,000TSH
MATUMIZI YA MENDE
[a] Matumizi makubwa ya mdudu mende hutumiwa kama chakula cha mifugo kama bata, kuku,Samaki nk
[b] Pia mende anatumika kama chakula cha binadam hasa katika mataifa ya ASIA kama china,Thailand nk
[c] Pia mende hutumika katika mashuleni kama majaribio mbali mbali.
Kuna aina nyingi za mende duniani ila weng wetu tunaimani kua mende ni mdudu msumbufu na anatakiwa kuuwawa kwani ni mharibifu na msumbufu pia. Ila katika upande mwingine unaweza kuumtumia kama fursa ya kujiajiri mwenyewe na kujipatia kipato kwa njia ya ufugaji wa mende.
Ukiwa kama kijana mtaftaji na mjasiria mali nivyema ukajifunza zaidi juu ya ufugji wa mende toka kwa wataalam mbali mbali ili upate elim kwa kina juu ya ufugaji wa mende.
Nikweli kabisa mende wanalipa japo katika jamii yetu uwe tayari kupokea shutuma zozote juu ya swala hilo kwani wengi wanaamini kua mende si mdudu anae staili kufugwa hata mara moja na pindi tu aonekanapo bas anatakiwa kuuwawa.
Kwaleo naomba tuishe hapo makala ijayo tutaangalia Aina za mende na jinsi ya kufuga mende.

image

Install Palscity app