3 yrs - Translate

Unataka kuanza Biashara au una mtu anataka kuanza Biashara?

Mpe huu ukweli ambao haujui??‍♂️

Kuanza Biashara kuna Phase ambazo kila mtu hupitia, jifunze kupitia hizi kabla hujaanza Biashara;

*Phase 1;* Hapa ni pale ambapo una hamu na shauku ya kufanya biashara halaf haujui hata kuanza, hujui hata biashara yenyewe, hapa utapata kelele nying za nje, kila mmoja atakushauri biashara yake, yaani utafollow wahamasishaji kibao, hamasa inaamka, nguvu tele, unajion tayar ushakuwa tajiri, unawaza kila biashara unaiweza??.

Hii phase wengi hukosea kwa kufuata mkumbo na sio kufata wao wenyewe nn wanataka, wanajisahau.

*Phase 2;* Sasa ukifaulu ile phase ya kwanza kwa kufata moyo wako nini unahitaji, kugunduwa lengo lako la maisha na kujuwa nani unataka kuwa inakupelekea kugunduwa unapaswa kufanya biashara gani kufika pale unapotaka kufika au kuwa unavyotaka kuwa.

Na hapa kinachofata ni kutafuta maarifa kabla hujaanza Biashara unayotaka kufany, lipia mafunzo ya biashara, soma vitabu, tafuta mentor akuongoze.

Ila kuna wale wanofata mkumbo sasa, wao kwenye phase hii huruka, badala ya kutafuta maarifa wanaenda kuanza moja kwa moja Biashara wanakuta mambo tofauti, wanapigwa, wanakata tamaa kabisa.

*Phase 3;* Hii kwa wale ambao waliwin phase ya zilopita hapa sasa wankuwa vizur, wanaanza kufanya Biashara baada ya kujipika kwa mda. Tayari wanakuwa na lengo, mpango na njia za kufanya yaani wao wanaenda hawana tabu mdogomdogo.

Kwa wale ambao walifeli zilopita hapa wanaanza kulalamika sasa na kuzani wale wenzao walibahatika tu kuamini kuwa kila mmoja ana bahati yake.

*Phase 4;* Wale walowin kama kawaida sasa washaingia sokoni, washakutana na changamoto nying sana katikati, ila kwa vile wana mentors wao wamesonga mbele na wametatuwa changamoto zote na tayari wanaendelea kujifunza na kukuwa zaidi.
Hizo process ni zaidi ya miaka 5 niamini.

Mafanikio siku zote ni mchakato
__

By Nassir Shariya
Mwl. Wa Biashara na Ujasiriamali mitandaoni.

Install Palscity app