4 yrs - Translate

ELIMU HUONGEZA (UPEO) FIKRA ZA KUFIKIRI

Fikra ni kitu muhimu sana katika maisha ya mwanadanu yeyote, kwani akili na utashi humwezesha kuishi na kufanya maamuzi ya kimaisha. Kwa kuwa kila mtu amezaliwa akiwa na akili timamu hivyo elimu huongeza upeo wa kufikiri na humpa mtu nafasi ya kufanya maamuzi magumu ya kimaisha kwa usahihi na ufanisi wa hali ya juu.
Kwa njia hii watu wengi wamekuwa na maarifa ya aina nyingi yanayowafanya wafikiri kwa viwango vya juu kuliko hapo awali, na tuwekeze katika elimu ili tujikwamue kimaisha.
Maisha ya msomi na mtu asiyesoma ni tofauti kabisa kwani msomi ana upeo mkubwa wa kufikiri na wa kukabiliana na changamoto za kimaisha kuliko mtu asiye na elimu ya kutosha.

Install Palscity app