WEMA WANGU UMENIPONZA - 2
Author : BAHEBUZA
Basi ikawa balaa kwa Fideli Castol akataka kunifunika nikamzuia badala yake nikamsogelea na kumkumbatia kwa nguvu huku nikihema kwa nguvu Fidel akiwa haelewi kitu maana hatukuwahi kuvunjiana heshima hata siku moja hivyo ikawa ajabu kwake .Basi nikajikuta namuomba Fidel Castol mapenzi huku nikiwa nimelegeza macho yangu huku nimembana kwa nguvu asitoke . Haikuwa kazi rahisi nilitumia nguvu sana kuitafuta koki yake na hatimae kuanza kuichezea huku Fidel akiwa anakosa ujanja na kuamua kushirikiana nami sio siri kwa mara ya kwanza niliingia mapenzini na mwanaume yule daah nae alijua kunipiga mpaka mtoto wa kingoni kuwa hoi huku nikivuja jasho huku macho yakiwa yamelegea kwa shughuli ya Fidel Castol Enginear wetu wa kazini kwetu.Baada ya mchezo ule wa uzinzi nikamuomba Fidel twende tukaoge nae kukubali kwenda kuoga pamoja na baadae tulijiandaa na kuingia kazini huku tukiwa wepesi lakini tu hatukuweza kuonana na Fidel kwa kuwa yeye alikuwa na kazi zaidi za nje ofsini hakuwepo sana. Lakini ajabu sana siku hiyo nilijikuta nasinzia tu ofisini tofauti na siku zingine zozote hali ambayo ilimfanya kila mtu kuniuliza kulikoni kuwa vile hivyobasi nilikosa jibu na kuishia kucheka tu huku nikikumbuka kipigo cha pweza na staili ya sokomoko aliyonipa Fidel Castol asubuhi mmh kilinifanya nichanganyikiwe ukizingatia ni siku nyingi sana sijashiriki michezo ile na huu ndiyo wa kwanza na huyu kaka Fideli Castol . Nilijikuta nampenda zaidi Fideli Castol kiasi cha kuingiwa na wivu mkali sana juu yake hali ambayo hata yeye aliigundua wazi . Sasa basi baada ya kile kipigo Fideli Castol alikuja tena kunipa kipigo kingine cha kufa mtu siku hiyo alilala kabisa kwangu ilikuwa ni siku ya Jumamosi kuamkia jumapili nakumbuka usiku wa saa 4 ndipo tulipoanza mambo yetu ilikuwa patashika alinikoleza mpaka nikachanganyikiwa na roho yangu kiukweli alinijulia sana kunitandika . Sikusita kumuomba tufunge ndoa kwani niliona ndiye mwanaume peke anayenifaa kwa muda ule hakukuwa na ubishi nilishampenda Fideli Castol sikuangalia imani zetu za kidini .Ajabu sana Fideli Castol safari hii alinikubalia ombi langu la kufunga nae ndoa na tayari alikubali kubadilisha imani yake ya dini jambo ambalo sikuliamini lakini ukweli ulibakia vile na hatimae shughuli kuanza mara moja huku wafanyakazi wenzetu wakituchangia michango mikubwa . Hatimae ndoa ikafungwa nyumbani kwetu songea na sherehe zingine kuja kumalizikia Mkoa wa iringa huku wafanyakazi wenzetu wakitusapoti kwa hali na mali . Baada ya ndoa yetu mie nilihamia Mkwawa nyumbani kwa Fideli Castol na kuanza kuishi kama mke na mume huku maisha yetu yakiwa na amani na furaha kubwa sana kwani kila mmoja wetu alimpenda sana mwenzie hali ambayo ilizalisha mawada makubwa sana ndani ya ndoa yetu.Huku kila mmoja wetu akiamini mwenzake ndiye Faraja yake sikuhisi kitu chochote kibaya kuhusu maumivu makali juu ya wema wangu kwa kiumbe mwenzangu kunitenda unyama kweli Maumivu ya moyo hayapoi kwa sindano ya ganzi . Maisha yaliendelea nami kuzidi kubadilika na kuwa mrembo zaidi Kutokana na kuridhika na hali ya ndoa yetu na Mume wangu Fideli Castol au Fahad kila mtu alituonea wivu Kutokana na tulivyoishi kwa kuelewana na hata kupendana kidhati bila kuficha hisia zangu za mahaba yangu kwake . Hatimae tulijaaliwa mtoto wa kiume ambaye tulimwita Ramcey hali ambayo ilizidisha Mapenzi makubwa sana kwa mume wangu Fideli Castol au Fahad nikajiona ni mmoja wa Malikia wenye bahati ya hali ya juu katika dunia hii sikufikiria maumivu yoyote juu ya Mapenzi na kuweka hisia zangu labda wale wote wanaoumizwa ni wale wasiojua wajibu wao katika kulinda Mahusiano yao na wapenzi wao . Kiukweli niliwaona wapuuzi sana kulalamikia usaliti wakati wapenzi wa kweli wapo mfano mzuri akiwemo Fideli Castol mume wangu Kipenzi ambaye nilimpenda sana kuliko hadith yoyote ile .
Maisha yaliendelea siku mpaka siku sasa siku moja nikaamua kwenda nyumbani Songea huku nikiwa na mume wangu Fideli Castol maana ilipita muda mrefu sana kuwatembelea wazazi wetu tulienda Songea na usafiri wetu wa binafsi na tulikaa kama siku tano hivi pale nyumbani huku jamaa na ndugu na marafiki zangu mbali mbali wakija kunisalimia na kumsalimia mume wangu Kipenzi Fideli baaada ya kumuona miaka kama 12 iliyopita nyuma yetu umri wa mtoto wetu Ramcey .Katika marafiki zangu hao alikuwepo swahiba yangu kipenzi
Consolata Saimon Alex ambaye alikuwepo hapo nyumbani songea akiwa hana kazi yoyote ya kufanya akiwa dada wa kupendeza na kunywa bia za watu huku akiwatapeli wanaume mbali mbali mapenzi yaani Conso alikuwa mchafu wa tabia mbaya za uongo na tamaa sana hakupenda kabisa kujitengenezea wema na watu wa jamii yake aliishi maisha ya kujikweza sana na kujiona mjanja na mwenye akili Kutokana na kufanikiwa sana mambo yake mengi ya kipuuzi . Sasa basi Kutokana na kuchoka kuishi pale Songea akaomba tuondoke pamoja na kuja kuishi nae Mkoa wa iringa . Daaah nilifurahi sana wazo lake nilijua tutakuwa ndugu watatu sasa Mkoa wa iringa ukiacha dada yangu Nasra aliyeolewa na Salim Hashim lilikuwa ni ombi la haraka sana nami sikuchelewa kumfahamisha mume wangu Fideli Castol habari zile kwani ndiye mwenye nyumba na mamlaka yote ya utawala hali ambayo haikuwa ngumu sababu Consolata Saimon alikuwa rafiki yangu tangu utotoni hivyobasi tulicheza na kufanya mengi sana pamoja kama ndugu kumbe majirani tu wa mtaa mmoja. Lakini kabla ya kuondoka kuja huku Iringa nilimuasa aachane na mambo ya kunywa pombe na kuvaa nguo za hovyo hovyo kwani sio vizuri kwa binti wa kitanzania aliyelelewa kimaadili na wazazi wake kwani ni jambo baya sana kwa binti kunywa pombe kwani pombe ni hatari Kutokana na vishawishi mbali mbali toka kwa wanaume na hata kubakwa na kuambukizwa magonjwa ya zinaa na virusi vya ukimwi . Pombe hata katika amri kumi za Mungu imekatazwa kwa imani zote za kidini sababu ina madhara na haileti faida yoyote kwa familia zaidi ya hasara tu .Consolata alinielewa na akaanza kubadilika haraka sana hali ambayo ilimshangaza kila mtu pale mtaani na nyumbani alianza kupendeza sana kiasi ambacho hata mie nilimuonea wivu Kutokana na urembo wake Consolata alikuwa mrefu halafu ana shape la umbo la nane huku akiwa na hipsi pana na makalio manene ambayo kila akivaa suruali zilimkaa vizuri alikuwa na jicho kubwa la kupakia wanja na vidimpozi mashavuni kiukweli alikuwa mrembo sana . Sasa basi kila alipokuwa anakuja pale nyumbani kwetu yaani kwa mzee Said Ubwa mume wangu Fideli Castol hakuacha kabisa kumuangalia
Consolata huku Conso nae akilegeza macho kwa shemeji yake hali ambayo haikuwa nzuri kabisa nilihisi itakuja kuleta hatari kubwa lakini nilipuuza tu sababu ilikuwa ni dhana tu sio kweli lakini kama ningejua ya mbele yangu hakika nisingemchukua Consolata na kuja kuishi nae Mkoa wa iringa huwezi kujua vyote vya ndani ya moyo wa binadamu kwani moyo wa mtu ni kichaka kumjua mtu kazi sana ndugu zangu.
Basi tulikaa kama wiki mbili mbele na hatimae kuanza safari yetu ya kurudi nyumbani kwetu Mkoa wa iringa huku tukiwa na Consolata na mtoto wetu wa pekee Ramcey ilikuwa ni familia mpya yenye upendo na maelewano . Consolata alianza kumheshimu sana shemeji yake Kutokana na kumpa somo la kiutu uzima naye kunielewa vyema na kuutumia vyema ushauri ule . Alibadilika sana na kuwa binti wa kueleweka hivyobasi Kutokana na kuwepo nyumbani alianza kushughulika na huduma mbali mbali za usafi wa nyumba na kuandaa chakula na hata kumfuatilia Ramcey kuhusu masuala mbali mbali ya shuleni hali ambayo ilitufanya tumpende na kumheshimu sana Consolata ,pamoja na hayo Conso alianza kuwa mrembo zaidi Kutokana na kujipamba kwani tulihakikisha nae anakuwa vizuri katika mavazi na urembo kama mwanamke . Consolata aliitumia vyema nafasi yake pale nyumbani kwetu alihakikisha anajua kila kitu cha pale na kukidhibiti zaidi ya yote alianzisha tabia ya kumfuatilia shemeji yake Fideli jambo ambalo aliliacha muda mrefu sana . Sababu ya kufanya vile ni Kutokana na muda mwingi sana kuwepo nyumbani halafu mie kuchelewa kurudi kutoka kazini nilianza kuhisi matukio mbaya kati ya Conso na mume wangu Fideli Castol kwani muda mwingi sana Consolata alikuwa akijiremba mida ambayo anajua Fideli Castol anarudi nyumbani hali ambayo mie nilianza kuishtukia baada ya kumkuta zaidi ya mara tatu akioga mida ambayo mume wangu anarudi nyumbani halafu akishaoga hukaa sebuleni na kuanza kuchat na simu kumbe kwenye simu yake alikuwa ana chati na shemeji yake yaani mume wangu Fideli Castol niliigundua siku ambayo aliiacha simu yake sebuleni nae kuingia chooni huku akiiacha wazi niliichukua na kuzisoma meseji zote za mume wangu alizomtumia rafiki yangu Consolata nami kuirudisha simu ile pale pale ili asijue kama nmegundua mchezo wake dhidi ya mume wangu Kipenzi Fideli Castol:
TUTAENDELEA SEHEMU YA TATU .