WEMA WANGU UMENIPONZA - 1
Author : BAHEBUZA
Naitwa Naima Saidi nimezaliwa Songea na kukulia huko ila maisha yangu nimeyapatia Mkoa wa iringa mpaka leo hii nikiwa mlemavu wa miguu kisa kutetea penzi langu kwa mume wangu Fideli Castol ambaye alikuwa mfanyakazi wa Tanesco mkoa wa Iringa . Kilichonifanya niumie na kusimulia mkasa huu wa ukweli wa Mapenzi ni kuhusu Wema wangu ambao nilimfanyia ndugu yangu rafiki yangu tuliyecheza nae utotoni Consolata Saimon Alex nae kunitendea unyama wa kutisha na kusahau kabisa hisani zangu juu yake . Sikuamini wala akili yangu haikutaka kukubaliana kirahisi tukio alilonifanyia Consolata dhidi ya mume wangu Kipenzi Fidel . Simulizi hii inaanza hivi :-
Baada ya mie kumaliza elimu yangu ya msingi nyumbani songea Dada yangu Nasra alinichukua ili kuniendeleza kielimu kwani mzee wetu mzee Said hakuwa na uwezo zaidi ya kumudu mahitaji ya chakula tu pale nyumbani ,na katika familia yetu tulizaliwa wanawake wawili tu mie na dada yangu Nasra basi hatukuwa na ndugu mwingine baada ya kuzaliwa mie Dada Nasra aliolewa na Salim Hashim ambaye alikuwa mfanyakazi wa kiwanda cha Maji Africa kama mtu wa masoko hivyobasi hawakuwa vibaya kimaisha kwani hata dada yangu Nasra nae alikuwa mfanyakazi wa Idara ya Maji mkoa wa Iringa wote hawa walikuwa wapo vizuri hali ambayo ilimpelekea dada yangu Nasra kunichukua ili wanisaidie kielimu kuinusuru familia yetu ambayo ilikuwa vibaya katika suala la kipato.
Basi hatimae nikawa nimeondoka Songea na kuhamia Iringa kwa shemeji Salim na dada yangu Nasra na bila kuchelewa kupelekwa shule kuanza form one .Dada na shemeji walikuwa wamejenga maeneo ya Wilolesi huku kila mmoja wao akimiliki usafiri wake kwa ajili ya shughuli mbali mbali za mjini . Kwa kuwa nilikuwa na malengo yangu nilikazana kusoma kwa bidii sana na hatimae kufaulu kuendelea na masomo ya Chuo kikuu cha Ruaha Catholic University RUCU nikisomea masomo ya Recording Management na kufaulu vizuri sana hali ambayo ilimpelekea dada yangu Nasra kufurahi zaidi hivyo basi tukaanza mchakato wa kutafuta ajira hatukuchelewa kupata ajira katika shirika la umeme la Tanesco mkoa wa Iringa huku nikiwa Recording Management wa shirika hilo na kulipwa vizuri sana . Sasa basi wakati nimeanza kazi tu ndipo hali ya vishawishi vya mapenzi vikaanza dhidi yangu kutokana na kujichanganya sana na Kampani za wanaume kaazini hapo . Sio siri nilipendwa na kila mwanaume wa kazini kwetu Kutokana na uzuri wangu wa sura na ukarimu Kutokana na asili yetu unajua wangoni ni watu wakarimu sana na wenye adabu sana hasa wanawake hilo nilijaaliwa sikulewa sifa ya kusifiwa uzuri wangu nilifuata maagizo ya malezi bora ya wazazi wangu juu ya kuwatendea na kuwafanyia
Wema watu mbali mbali ninaowajua na nisiowajua katika dunia hii ambayo binadamu huwezi kujua kesho atakusaidia nani haya yalikuwa ni maneno ya mama yangu kila siku tulipokaa nyumbani . Sasa katika hilo ndipo alipotokea katika mmoja hivi ambaye alikuwa Enginear hapo kazini kwetu aliitwa Fideli Castol kaka huyo alikuwa mpole sana na mwenye hekima hakuwa na maneno ya kipuuzi wala ujinga jinga hapo kazini mara nyingi sana alipenda kusoma vitabu mbali mbali vya masuala mbali mbali ya teknologia hali ambayo ilinivutia sana mie na hata mara nyingi sana kumwazima vitabu nami nisome . Lakini katika wanaume wote wa pale kazini kunitongoza Fideli hakuwahi kuniambia kuhusu kunitaka japo kuwa mie nilianza kuvutiwa nae Kutokana na kuwa Gentlemen lakini sikufaulu kufikisha ujumbe wangu kwa Fidel Castol basi siku zilienda huku maisha yakiendelea nami kuzidi kubadilika na kuwa binti mrembo zaidi ya mwanzo kwani pesa yangu ya mshahara ilikuwa nzuri sasa kutokana na kuona sasa naweza kuishi mwenyewe nikamuomba dada yangu Nasra ruhusa nikapange ili niweze kujifunza zaidi maisha ,Daah ilikuwa kazi kubwa sana kumshawishi dada yangu Nasra kukubali mie nikapange lakini hatimae baadae alielewa na kuniruhusu huku wakinipa baadhi ya sapoti ya kuanzia maisha . Basi nikawa nimeanza maisha yangu ya kujitegemea mwenyewe nilipanga maeneo ya Ilala huku Fidel Castol akiwa anaishi maeneo ya Mkwawa hali ambayo ilipelekea kila mara kunipa lift ya pikipiki yake mara tu anaporudi nyumbani kwake.
Mara zote hizo Fidel hakuonyesha dalili zozote za kunitaka japo kuwa mie nilishaanza kujishebedua kwake si unajua tena sie wanawake tukiwa tunataka kitu hatuishiwi vituko basi sikuacha kumfanyia vituko kila alipokuwa ananiacha nyumbani nilipokuwa nimepanga nae kwenda kwake Mkwawa ilikuwa desturi sasa kila siku lazima Fideli aje kunichukua pale nyumbani na kuelekea pamoja kazini hali ambayo ilimfanya kila mmoja wa wafanyakazi wenzetu kuanza kuhisi vingine ,Kumbe daah haikuwa vile Kutokana na Fidel Castol kuwa mgumu wa kuelewa hisia zangu za mahaba yangu kwake sababu tu ya ule ukimya wake .
Muda mrefu sana ulipita bila kuonana na mwanaume kimapenzi hivyobasi kama binadamu niliyekamilika nikaanza kujihisi vibaya kwani sikuwa na mwanaume yoyote kimapenzi niliishi peke yangu tu Kutokana na kuogopa sana mahusiano ambayo yataniumiza moyo wangu kutokana na mifano niliyokuwa naipata kwa marafiki zangu waliobahatika kuolewa na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wao . Halafu jingine sikuwa na tabia mbaya ya kimalaya Kutokana na kulelewa katika familia ya kiimani yaani malezi ya kiislam Kutoka kwa wazazi wetu tangu tukiwa wadogo kwani tulikuwa tukisoma madrasa na kujistiri mpaka leo hii hali ambayo ilimfanya dada yangu Nasra aolewe na Salim Hashim baada ya Salim kumuona dada yangu Nasra akiwa anaenda kusali na kwenda madrasa . Salim alikuwa amekuja kwa baba mdogo wake Ally aliyekuwa anaishi Songea . Siku ambazo alikaa pale Songea zilimfanya amchunguze kwa kina kabisa dada yangu Nasra na kumjua vyema kitabia na hatimae kufanya mipango ya kumuoa na kuja kuishi nae Mkoa wa iringa . Hali ya Fidel kutokuelewa nini nahitaji kwake ilidumu muda mrefu sana hatimae nikaanza kukata tamaa na Fidel Castol kwani hakuonyesha dalili zozote za kunitaka kimapenzi nikaamua kufanya subra tu mpaka hapo atakaamua mwenyewe huku Dada Nasra na shemeji Salim wakiniuliza kama nshapata mchumba suala ambalo liliniumiza sana kichwa changu kwani nilihitaji sana mtu wa kunikumbatia na kunidekeza nilitamani sana kwani niliwaonea wivu dada Nasra na shemeji yangu Salim walivyokuwa wakicheza kukumbatiana na hata kwenda kuoga pamoja bafuni na mengineyo mengi tu ya kikubwa ambayo kwa umri wangu nami nilihitaji sana kufanyiwa yale na ndiyo maana nikaomba nikapange nje ili nimpate mtu wangu wa kunistiri lakini sikumpata hata yule niliyekuwa namfikiria nae hakuwa na time na mie kiukweli niliumia sana roho mbaya zaidi pale nyumbani kila mdada alikuwa akiishi na mume wake nilichoumia zaidi kuna siku usiku mpangaji wa chumba cha jirani yangu alikuwa analakamika sana kwa utamu wa Mapenzi aliyokuwa akipewa na bwana wake sauti ambayo ilipenya moja kwa moja mpaka ndani ya moyo wangu na kuivuruga kabisa akili yangu kutokana na hali ya matamanio ya mchezo ule wa Mapenzi uliyokuwa ukiendelea chumba cha jirani yangu Maimuna na bwana wake Maliki Mgidange kiukweli walinitesa sana kihisia kiasi cha kuinyanyasa nafsi yangu.
Basi siku ya pili yake yaani asubuhi wakati wa kwenda kazini kama kawaida Fideli Castol alikuja kunichukua lakini hakuingia sebuleni daah basi ikabidi siku hiyo nimchezee mchezo ili anipe japo kidogo tu kwani hali yangu haikuwa nzuri kabisa nilihisi kuja kudata Kutokana na hali ilivyokuwa mbaya ,basi nikajifanya naumwa sana tumbo huku nikijinyonganyonga pale sebuleni hali ambayo ilimpelekea Fidel Castol kuamua kuingia sebuleni kwangu ili ajue jinsi ya kunisaidia daah nilikuwa niko kimtego sana hata nguo ya ndani sikuwa nimeivaa basi nikajifanya naumwa sana tumbo huku nikipiga kelele za maumivu makali . Fideli Castol kuona vile akaanza kutaka kuninyanyua ili twende hospitalini nikamkatalia na badala yake nikamuomba anipeleke chumbani kulala masikini hakuujua mtego wangu basi akanibeba mpaka chumbani na kunilaza juu ya kitanda huku nguoniliyoivaa kimtego ikiachia sehemu kubwa ya mwili na kuonekana yalikuwa ni maeneo ya mapajani kuelekea ikulu nikaona Fideli Castol kakaza macho sehemu zile huku jasho zikianza kumtoka asubuhi ile ilikuwa ni hali ya hatari sana kwani nilikuwa nimejaaliwa sana maeneo ya kiuno matakoni na miguuni na rangi yangu nyeupe ya kingoni na kinyamwezi basi daah ikawa balaa.
TUTAENDELEA SEHEMU YA PILI