Ni katika sherehe ya harusi, mchungaji aliuliza ikiwa kuna mtu yeyote yule ambaye alikuwa na sababu yoyote kwa nini tu ndoa hiyo isiendelee na ilikuwa wakati wa kusimama na kusema, au lah milele waachwe wanyamaze kwa amani.
Ikawa kipindi cha ukimya kabisa kilikatizwa na mrembo aliyembeba mtoto. Akaanza kutembea taratibu kwa madoido kuelekea kwa mchungaji.
Kila kitu haraka kiligeuka kuwa machafuko. Bibi harusi alimpiga kofi la haja bwana harusi.
Mama wa bwana harusi akazimia. Msafara wa maharusi ukasonga mbele kuelekea mlangoni. Ndugu wa bwana harusi walikusanyika pamoja kama kundi lililofiwa, wakishangaa jinsi bora ya kusaidia kuokoa jahazi linaloelekea kuzama!
Punde, Mchungaji alimuuliza yule mwanamke: "Unaweza kutuambia kwa nini umejitokeza, una nini cha kusema?"
Mwanamke akajibu, "Sikuweza kukusikia vizuri kutoka nyuma ndio sababu nimesogea mbele."
SOMO: Shikilia hukumu mpaka upatapo ukweli wote. Na hata hivyo mara nyingi tunapiga risasi haraka sana na kusababisha mahusiano mema yanaharibiwa.
C&P