1 y - Translate

Kama ulikua hujui kuwa siku ya muungano kuna MWEMBE ulipandwa IKULU wacha nikufahamishe;-
Watu wengi wanajua tukio lililofanyika siku ya muungano,
Ni tukio la kuchanganya mchanga tu sio kweli,
Kuna matukio mengi yalifanyika kama kumbukumbu,
Na moja ya tukio ni kupanda MWEMBE IKULU,
Tena sio MWEMBE mwengine ni huo hapo chini,
MWEMBE huo ulipandwa IKULU jijini DAR ES SALAAM,
Ambapo NYERERE alipanda mche mmoja akiutoa kutoka TANZANIA BARA,
Na KARUME alipanda mche mmoja alioutoa ZANZIBAR,
Kisha wakatumbukiza miche yote miwili kwenye shimo moja,
Ambapo baadae wakati inakua iliungana na kutengeneza shina moja,
Na kuonekana kama unavyo uona hapo chini,
Tukio hilo la aina yake lilifanyika tarehe 26/4/1964,
Na lilifanyika masaa machache baada ya viongozi hao,
Kukamilisha tukio la kuunganisha nchi zao,
Na kuzaliwa jamhuri ya muungano wa TANZANIA,
MWEMBE huo hadi sasa upo IKULU jijini DAR ES SALAAM,
Na hujulikana maarufu kwa jina la MWEMBE WA MUUNGANO,
Na MWEMBE huo una mtu maalumu wa kuuhudumia,
Tangu ulivyo pandwa hadi leo hii ninavyo kuletea makala hii.

Makala hii imeletwa kwenu na Dhulkad Madara kutoka Morogoro

image

Install Palscity app