"QUR'AN NA FUNGA"
NI WAOMBEZI SIKU YA QIYAMA
عن عبدالله بن عمر -رضي الله عنهما- أنّه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم؛-
(الصِّيامُ والقرآنُ يشفَعانِ للعبدِ يومَ القيامةِ يقولُ الصِّيامُ أي ربِّ منعتُهُ الطَّعامَ والشَّهواتِ بالنَّهارِ فشفِّعني فيهِ ويقولُ القرآنُ منعتُهُ النَّومَ باللَّيلِ فشفِّعني فيهِ قالَ فَيشفَّعانِ)
MAANA YAKE
Kutoka kwa Abdillah bnu Omar..r.a kuwa Amesema Mtume s.a.w:
Funga na Qur'an zitawambea Mja siku ya Qiyama, Funga itasema ewe Mola nimemzuiya Kula na Shahwa mchana wa Ramadhani basi nawaombea kwa hilo.
Na QURAN itasema nimemzuiya kulala usiku basi namuombea kwa hilo
Basi vitamuombea
MAFUNZO YAKE
Tunapaswa kujifunza na Kuisoma QURAN usiku na mchana na kutekeleza yaliyomo ndani yake.!
Tunapaswa kuzitunza Funga zetu na Machafu ya Maneno na Vitendo ili Allah azikubalie na kutupa Ujira wake.!!