Biblia ina maagano (covenants) matano ambayo yote yana kiongozi wake, masharti yake, lugha yake, utekelezaji wake na ahadi zake.
Ukichagua kuishi ndani ya mojawapo jitahidi sana ulielewe linataka nini na halitaki nini, hii ndio njia pekee itakufanya ufanikiwe.
Kinachoumiza wengi hatuyajui maagano haya na ukimuuliza Mkristo Yeyote kama hajui atakuambia Biblia inayo mawili tu. Lakini ukweli yako matano
1. Agano la Mungu kwa Nuhu
2. Agano la Mungu kwa Ibrahimu
3. Agano la Mungu kwa Musa (La kale)
4. Agano la Mungu kwa Daudi
5. Agano la Mungu kwa Yesu (Agano jipya).
Ukitaka uione Biblia ngumu basi changanya vipengele vya agano moja kwa lingine bila kujua uhusiano uliopo.
Mfano Agano la Ibrahimu lina kutoa zaka kwa imani na hiari, mtoaji hupanga kiasi cha kutoa bila sharti wala kipengele kinachomuongoza zile asilimia huamua yeye kulingana na anavyompenda Mungu na hutoa kwa furaha kabisa (Ibrahimu, Yakobo walitoa hivyo). kwenye hili hautoi ili ubarikiwe unatoa kwa kuwa umebarikiwa tayari.
Agano la Musa (la kale) lina Zaka kwa lazima na mpokeaji zaka kapanga kiwango na ukitoa unabarikiwa usipotoa au ukitoa vibaya unalaaniwa.
Agano jipya limekuja kuondoa la kale nalo limekuja kwa amri zake na amri kuu ni upendo, Hili halitaki tulaaniwe linataka tubarikiwe na hili linataka tuungane na lile la Ibrahimu, kuhesabiwa haki kwa imani, NA HILI NDILO AGANO BORA KULIKO YOTE, LINALOTUONGOZA KWENYE UHURU WETU NDANI YA KRISTO.
SASA KAMA UKO NDANI YA KRISTO WEWE UMEKUWA HURU, UNAISHI NDANI YA BARAKA UNAZOZIPATA KWA IMANI, YA NINI KUJITIA TENA KWENYE AGANO LA UTUMWA LILETALO LAANA?
Nashauri usomaji wako wa Biblia ungejikita kujua unachosoma kipo chini ya agano gani, ingekusaidia sana kuelewa haki zako, wajibu wako, ahadi za Mungu kwako na ungeishi kwa amani na kumfurahia Bwana badala ya kuchanganyikiwa kila siku na elimu nyingi za kukuyumbisha.
Namshukuru Mungu nimekuwa na kundi la whatsap la watu zaidi ya 100, kwa mwaka sasa tukisoma sura kati ya 3,4 & 5 kila siku na tunamwona Mungu kwa usomaji huu. Anzisha tabia ya kusoma Neno la Mungu kila iitwapo leo kama unataka kuwa salama kwenye maisha haya yaliyojaa kelele nyingi za sauti nyingi.