TUJIFUNZE KUHUSU SARATANI YA KOO: (Cancer of the Esophagus)
Chanzo, Dalili na Tiba
Utangulizi
Saratani ya koo ni miongoni mwa magonjwa ya kutisha. Ingawa baadhi ya wagonjwa wa saratani ya koo wanaweza kutibiwa na kupona kabisa.
Vihatarishi vya kansa ya koo
Ingawa chanzo halisi cha kansa ya koo hakijulikani, mambo yafuatayo yanaweza kusababisha mtu kupata saratani ya koo. Hata hivyo, pamoja na kuwepo vihatarishi hivi, ni vigumu kueleza kwa ufasaha kwa nini mtu au watu fulani wanaweza kupatwa na kansa ya koo na mtu mwingine asipate. Vihatarishi hivi ni:
👉UMRI
Hatari ya kupata saratani ya koo huongezeka zaidi kwa watu walio na umri wa miaka 65 na kuendelea. Hata hivyo saratani ya koo aina ya adenocarcinoma inaweza kutokea hata kwa wanawake walio na umri kuanzia miaka 40 na kuendelea.
👉JINSIA.
Tafiti nyingi zimeonesha kuwa wanaume wana uwezekano wa kupata saratani ya koo mara tatu zaidi ya wanawake.
👉UVUTAJI WA SIGARA: Wavutaji sigara wapo katika hatari ya kupata saratani ya koo ukilinganisha na wasio wavutaji.
👉UNYWAJI WA POMBE KUPINDUKIA:
Unywaji wa pombe kwa kiasi cha chupa tatu na zaidi kwa siku unamuweka mnywaji katika hatari ya kupata saratani ya koo.
👉UNENE KUPINDUKIA: Unene wa kupitiliza huongeza uwezekano wa kupata saratani ya koo aina ya adenocarcinoma
👉TATIZO SUGU YA KUCHEUA TINDIKALI KUTOKA TUMBONI: , Hii huathiri sehemu ya chini ya koo na kusababisha hali ijulikanayo kitaalamu kama Barrett esophagus. Hali hii huongeza uwezekano wa kutokea kwa saratani ya koo.
DALILI ZA SARATANI YA KOO.
Mgonjwa mwenye saratani ya koo katika hatua za awali anaweza asioneshe dalili zozote zile. Hata hivyo, kadiri saratani inavyozidi kukua na kuenea, mgonjwa anaweza kuwa na dalili zifuatazo:
👉Chakula kukwama kwenye koo
👉Siku za mwanzo mgonjwa anaweza kushindwa kumeza chakula kigumu kisha cha majimaji na baadaye akashindwa kumeza hata mate
👉Maumivu wakati wa kumeza chakula hasa chakula kigumu
👉Maumivu kwenye kifua au mgongoni
👉Kupungua uzito
👉Kiungulia
👉Sauti ya mkwaruzo au kikohozi kikavu cha zaidi ya wiki mbili.
TIBA YA SARATANI YA KOO.
Saratani ya koo inaweza kutibiwa kwa kufanya upasuji,kutumia mionzi,kutumia kemikali maalum(chemotherapy) au.mchanganyiko wa vyote kutegemeana na athari ya saratani ya koo kwa sehemu nyingine za mwili.
LISHE NA SARATANI.
Lishe ni jambo la msingi sana kwa mgonjwa wa saratani ya koo kikuu cha saratani ya koo ni utapiamlo pamoja na upungufu wa kiwango cha sukari( hypoglycemia) unaosababishwa na magonjwa ya kushindwa kumeza chakula..hivyo ni muhimu kuzingatia lishe ya mgonjwa.Iwapo mgonjwa anshindwa kabisa kula daktari anaweza tumia njia mbadala kama vile kutumia bomba maalum la kupitisha chakula(feeding tube)
Ashraf Nassor
Delete Comment
Are you sure that you want to delete this comment ?