Elimu ni moja ya nyenzo muhimu ya kutatua matatizo katika jamii
Kila mwanadamu huishi kwa aina Fulani ya ujuzi unaomsaidia kupata kipato uitwao elimu. Ujuzi huu unatumika katika kuondoa umaskini na kutatua matatizo yanayoikumba jamii kama barabara, ujenzi, usafirishaji, kilimo n.k na elimu mbalimbali kama elimu ya ufundi, biashara, kilimo n.k hutatua matatizo hayo.
Kwa mantiki hiyo, ili matatizo mengi yatatuliwe katika jamii, aina Fulani ya ujuzi inahitajika eneo hilo; kwa mfano:- elimu ya mazingira husaidia kutunza rasilimali za taifa na kuongeza ufanisi wa kazi na maisha bora kwa wananchi kwa kutatua tatizo la ukame na njaa na mengineyo. Elimu ya udaktari huzifanya afya zetu kuwa imara muda wote ili tufanye kazi kwa ajili ya ujenzi wa taifa. Mwalimu anamuhitaji daktari na daktari anamhitaji mkulima kwa chakula ili aweze kutibu watu vizuri. Naam tunategemeana kiujuzi na kimaarifa.