@Barakasteven
Imekuwa ni tabia ya kawaida ya watu waliopo katika mahusiano kutumia muda mwingi kubishana kuliko kutulia na kusikilizana kuona wapi mmoja wenu anakosea ili kurekebisha penye tatizo na kuendelea kuishi kwa amani na upendo.
Jambo hili limekuwa likichangia kuwa na migogoro na majibizano yasiyo isha.
Kama hakuna anayekubali kusikiliza Kati yenu basi hakuna Jambo mtakalo amua kutatua mkafanikiwa.
Usitafute makosa kwa mwenzio wala usimuweke hatiani muda wote bali angalia ni nini kilicho ndani yake ambacho kinamfanya awe hivyo, kila mtu ameumbwa na kusudi ndani yake kwa hiyo makosa ni moja ya maisha ambayo anayapitia ili ajifunze, usimhukumu mtu kwa makosa yake bali jiulize kwanza ni nini sababu ya yeye kutenda kosa hilo.
Mtu yeyote ana kitu kinachomtofautisha yeye na mtu mwingine, hiko kitu ndicho kinamfanya ajivunie kuumbwa, kwa hiyo tusiangalie tu mabaya ya mtu, tuangalie pia ndani yake ni nini kipo kizuri.
Nawatakia usiku mwema, Mungu awabariki sana
Install Palscity app