Kama ulikua hujui kuwa unapo SAFIRI kuna mambo lazima uyazingatie wacha nikufahamishe:-
Watu wengi husafiri tu bila kujua kuwa kwenye safari,
Kuna mambo muhimu sana ya kuzingatia,
Mambo hayo ya kuzingatia ni haya yafuatayo:-
1). Salimia unayemkuta kwenye siti maana hujui ya baadae,
Inakera hukusalimia halafu baadae unaanza kumuuliza maswali,
Kwamfano:- eti hapa tumefika wapi ?, Sasaivi saa ngapi,
Wakati unakataa kumsalimia ulijue yeye mbwa au nyoka.
2). Kuwa mstaarabu unapoingia kwenye usafili,
Hasa kama tayari unajua siti yako haina haja ya kugombania mlangoni.
3). Sikiliza nyimbo na video za kwenye simu yako,
Kwa kutumia earphones kwani kinacho kufurahisha wewe kwa mwingine yawezekana ni kero.
4). Usiongee na simu kwa sauti kubwa,
Hasa mambo yako binafsi kwani hakuna anayehitaji kujua mambo yako,
Zaidi ya kuwa pigia kelele wenzio na kuwaletea usumbufu.
5). Kuwa mwangalifu unapo sinzia na epuka kumlalia jirani yako unaposinzia.
6) Unapo nunua gazeti na kuamua kulisoma,
Soma gazeti lako kwa uangalifu sio unalitandaza hadi linagusa pua ya mwenzako.
7) Usilazimishe kuchungulia dirishani kila mara,
Wakati umekaa siti ya katikati
hiyo ni kero kwa aliyekaa dirishani.
8). Kama unasafiri na watoto wakatie siti yao isiwe kero kwa jirani yako,
Unasafiri na watoto watatu kwenye siti moja,
Lazima utaleta kero kwa jirani yako na kwa watoto pia.
9). Usipende kujipulizia pafyumu yenye harufu kali,
Kwani hujui utakaa na mtu mwenye matatizo gani.
1 Hakikisha unapiga mswaki vizuri,
Kwani unapo safili huwa unakaa na watu karibu,
Ni kero kukaa na abiria anayenuka mdomo hasa anapokusemesha.
11). Msome vizuri abiria uliiyekaa naye Pamoja,
Kama hapendi kusemeshwa usimsemeshe semeshe,
Mwache wengine wana mambo yao kichwani,
Wengine wanaenda kwenye misiba na au kuuguza,
Wengine wamefukuzwa na waume zao huko walikotoka,
Sio kila mtu anapenda kuongea safarini.
12). Kama unajijua una tatizo la kutapika safarini,
Jiaandae mapema kwa kuwa na vifaa vya kukusaidia kwenye hali hiyo.
13). Punguza kula kula ovyo na kunywa vinjwaji laini,
Uwapo safarini hasa safari za mbali zaidi,
Ili kuepuka usumbufu wa kukojoa kojoa au kunyakunya hovyo njiani,
Dereva anaweza kukasilika akagoma kusimamisha gari,
Mwisho wa siku ukaanza kujinyea na kidhalilika.
14). Kijana kama kwenye Siti yako umepangwa na mtoto mzuri,
Mdada mrembo huyo ni mke wako pambana mpaka kieleweke,
Hakuna mke atakaeletwa na bwana mke analetwa na wewe.
15). Mdada kama una mwanaume mlevi mvuta bangi na limbukeni,
Bahati nzuri kwenye usafili na siti yako,
Ukawa umekaa na kijana smati na mcheshi,
Basi huyo ndiyo mume wako fanya haraka kumpa namba,
Halafu mambo mengine yatafuata polepole.
Makala hii imeletwa kwenu na Dhulkad Madara kutoka Morogoro