*MIAKA 100 KUANZIA LEO UNAJUA UTAKUWA WAPI? KAMA UNAJUA BASI JIPANGE ZAIDI NA KUMTAJA SANA ALLAH , IBADA, SADAKA NA ISTIGHFAAR NYINGI* *SUBUHANNA LLAH, ALHAMDULILAH, ALLAH AKBAR*
وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّهِ وَكِيلًا
(AL-AH'ZAB - 3)
Na mtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni wa kutegemewa.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّهَ ذِكْرًا كَثِيرًا
(AL-AH'ZAB - 41)
Enyi mlio amini! Mdhukuruni Mwenyezi Mungu kwa wingi wa kumdhukuru..
وَسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا
(AL-AH'ZAB - 42)
Na mtakaseni asubuhi na jioni.
HARUFU YA MFUNGAJI NI MISKI MBELE YA ALLAH
قال رسول الله عليه الصلاة والسلام
(وَالّذِى نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لَخُلُوفُ فَمِ الصَّائِمِ أَطيَبُ عِندَ اللَّهِ مِن رِيحِ المِسكِ)
MAANA YAKE
Amesema Mtume s.a.w
Naapa kwa yule Nafsi yangu ipo katika miliki yake:-
Hakika Harufu ya Mdomoni wa Mfungaji ni nzuri zaid mbele ya Allah kuliko hata Harufu ya Miski.
MAFUNZO YAKE
Miongoni mwa Fadhila na Utukufu wa Funga..kuwa harufu inayobaki mdomoni mwako ni Miski mbele ya Allah.
Tumbo Kukosa chakula na kinywaji mchana wa Ramadhani ni faida kubwa ya kuutengeza mwili wako kiafya na kiimani.
FUNGA SIO KUJIZUIYA NA KULA NA KUNYWA TU
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم :
( ليس الصيام من الأكل والشرب إنما الصيام من اللغو والرفث فإن سابك أحد أو جهل عليك فقل إني صائم إني صائم )
رواه ابن خزيمة
MAANA YAKE
Kutoka kwa Abi Huraira R.a amesema..amesema Mtume s.a.w:-
Sio Funga Kujizuiya na Kula na Kunywa lakini ni kujizuiya na Mchafu na Maovu,
Na kama mmoja akikutukana au kukudharau tu basi sema kumwambia mimi ni nimefunga Mimi nimefunga
Kaipokea: Ibnu Khuzaimah.
MAFUNZO YAKE
Funga ya kweli ni kuacha Maovu na Machafu ya Vitendo ama Maneno.!!
Usilipizane na mwenzako kwa Uovu bali sema tu kwa Busara NIMEFUNGA..!
UKARIMU NA UPOLE NDANI YA RAMADHANI:
عن عبدالله بن عباس رضي الله عنهما
( كَانَ رَسُولُ اللَّهِ أَجْوَدَ النَّاسِ وَكَانَ أَجْوَدُ مَا يَكُونُ فِي رَمَضَانَ حِينَ يَلْقَاهُ جِبْرِيلُ وَكَانَ يَلْقَاهُ فِي كُلِّ لَيْلَةٍ مِنْ رَمَضَانَ فَيُدَارِسُهُ الْقُرْآنَ فَلَرَسُولُ اللَّهِ ع أَجْوَدُ بِالْخَيْرِ مِنْ الرِّيحِ الْمُرْسَلَةِ)
MAANA YAKE
Kutoka kwa Abdilaah bin Abaas R.a..
Alikuwa Mtume saw ni mzuri ktk watu, na vizuri zaidi alipokuwa ktk mwezi wa Ramadhani pindi alipokuwa akiijiwa na Jibril kila usiku wa Ramadhani na kufundishwa Qur'an, na alikuwa ni mwepesi wa kufanya mambo ya kheri kuliko upepo
MAFUNZO YAKE
Ukarimu unahitajika kila wakati na Hassa mwezi wa Ramadhani kusaidiyana na kutatuliyana Shida zetu.!!
Ni kipindi kitukufu cha Kudarisi na Kujifunza zaidi Kitabu cha Allah na hata kuwafunza wenzako.!!
"QUR'AN NA FUNGA"
NI WAOMBEZI SIKU YA QIYAMA
عن عبدالله بن عمر -رضي الله عنهما- أنّه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم؛-
(الصِّيامُ والقرآنُ يشفَعانِ للعبدِ يومَ القيامةِ يقولُ الصِّيامُ أي ربِّ منعتُهُ الطَّعامَ والشَّهواتِ بالنَّهارِ فشفِّعني فيهِ ويقولُ القرآنُ منعتُهُ النَّومَ باللَّيلِ فشفِّعني فيهِ قالَ فَيشفَّعانِ)
MAANA YAKE
Kutoka kwa Abdillah bnu Omar..r.a kuwa Amesema Mtume s.a.w:
Funga na Qur'an zitawambea Mja siku ya Qiyama, Funga itasema ewe Mola nimemzuiya Kula na Shahwa mchana wa Ramadhani basi nawaombea kwa hilo.
Na QURAN itasema nimemzuiya kulala usiku basi namuombea kwa hilo
Basi vitamuombea
MAFUNZO YAKE
Tunapaswa kujifunza na Kuisoma QURAN usiku na mchana na kutekeleza yaliyomo ndani yake.!
Tunapaswa kuzitunza Funga zetu na Machafu ya Maneno na Vitendo ili Allah azikubalie na kutupa Ujira wake.!!
Ni MTU mpole mkalimu na nisie na makuu... Sio mtu wa kila mtu,,, lakini Ni MTU wa watu.
Install Palscity app