Katika ukurasa wetu wa leo tutaona ugonjwa wa UKIMWI ni nini na zipi ndizo dalili za ugonjwa huu. UKIMWI (Ukosefu Wa Kinga Mwilini) ni ugonjwa unaosababishwa na VVU (Virusi Vya UKIMWI). UKIMWI hudhoofisha mfumo wa kinga za mwili na kumfanya mtu aweze kuambukizwa au kupata magonjwa mbalimbali. Uwezo wa mwili wa kujikinga na maradhi hupungua zaidi kadri ugonjwa wa UKIMWI unavyoongezeka ndani ya mwili wa mgonjwa.
Mtu mwenye virusi vya UKIMWI tunasema ameathirika. Virusi vya UKIMWI hushambulia seli za T (T-cells) katika mfumo wa kinga za mwili. Mara nyingi mtu mwenye virusi vya UKIMWI atapata ugonjwa huu wa UKIMWI lakini si kila mtu aliye na virusi vya UKIMWI ana ugonjwa huu. UKIMWI ni ugonjwa na mtu anakuwa na
UKIMWI pale ambapo virusi vya UKIMWI alivyonavyo ndani ya mwili vimefikia hali ya kudhoofisha kinga zake za mwili na mwili kushindwa kuzuia maradhi mengine yanayounyemelea. Mtu aliye na virusi vya UKIMWI baadaye huupata ugonjwa huu na asipotumia dawa, hufariki dunia.
Utafiti sasa unaonyesha kuwa ugonjwa ulianza miaka ya mwishoni mwa karne ya 19 na ya mwanzoni mwa karne ya 20 na utafiti huo unaonyesha kuwa ugonjwa huu ulianzia Afrika Ya kati na Afrika Magharibi. Mgonjwa wa kwanza alibainika kuwa na ugonjwa huu mwaka 1980.
Hadi sasa hakuna dawa ya kuondoa UKIMWI bali kuna tiba za kupunguza makali ya ugonjwa na kumsaidia mgonjwa kuongeza uhai wake. Baadhi ya watu waliotumia tiba hizi wameishi muda mrefu na maisha ya kawaida.
Ugonjwa unaweza kugundulika katika hatua zake za mwanzo kabisa hivyo kumsaidia mgonjwa kuweza kuanza kupata tiba ya kuzuia virusi kuongezeka kwa haraka katika mwili wake na hivyo kurefusha muda wake wa kupata UKIMWI. Mgonjwa anayetumia dawa za kurefusha maisha bado ana virusi hivi na anaweza kuambikiza
watu wengine.
UKIMWI UNAAMBUKIZWA VIPI?
VVU (Virusi Vya UKIMWI) hupatikana ndani ya majimaji yaliyomo mwilini mwa mgonjwa huyu, ikiwa ni ndani ya shahawa za mwanamme, damu na maziwa ya mama. Ugonjwa huu huambukizwa pale damu ya mtu inapokutana ana kwa ana na damu ya mtu aliyethirika au kwa ngono. Vile vile mama mwenye UKIMWI huweza kumuambukiza mwanae aliye tumboni wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua au kwa kumnyonyesha maziwa.
Ugonjwa wa UKIMWI huambukizwa pia kwa kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo, kufanya mapenzi kinyume na maumbile, kuongezewa damu isiyo salama na kupitia sindano ambazo si salama.
Dalili Za UKIMWI
Watu wengi wenye virusi vya UKIMWI hawaoni dalili zo zote kwa miaka kadhaa. Wengine hupata mafua kati ya wiki mbili hadi sita baada ya kupata maambukizi ambayo hudumu kwa kipindi cha hadi wiki nne. Dalili nyingi zinazotokea zinatokana na maambukizi ya bacteria, virusi, fungus na wadudu wengine.
Dalili za awali za UKIMWI ni kama zifuatazo:
. Homa
. Kusikia baridi
. Maumivu ya joints
. Maumivu ya misuli
. Koo kavu
. Jasho (Hasa usiku)
. Uchovu wa mwili
. Udhaifu
. Kukonda
Baada ya dalili hizi za awali kutoweka, mara nyingi hakuna dalili zo zote zitakazooneka kwa kipindi kirefu. Wakati huu wadudu hawa wanazidi kuzaliana, kuongezeka na kuharibu mfumo wa kinga za mwili. Kipindi hiki cha ukimya kinaweza kwenda hadi miaka 10 wakati huu wote mtu akijisikia vizuri tu na kuonekana mwenye afya.
Dalili za mwisho za UKIMWI zinaweza kuwa:
. Kutoona vizuri
. Kuharisha mfululizo
. Kikohozi kikavu
. Homa kali inayokwenda kwa muda mrefu
. Kuvuja jasho usiku
. Uchovu wa mwili mfululizo
. Kupumua kwa shida
. Kukonda
. Vijidoa vyeupe kwende midomo na ulimi
Mtu anapofika kwenye hatua hii na kuanza kuonyesha dalili hizi, anaweza sasa kunyemelewa na gonjwa lo lote linaloweza kumuua. Magonjwa hayo nyemelezi ni kama:
. Esophagitis (matatizo kwenye ngozi laini ya kooni)
. Maambikizi kwenye mfumo wa neva (acute aseptic meningitis, subacute encephalitis na peripheral neuropathy.
. Pneumonia.
. Kansa kama za Kaposi’s sarcoma, kansa ya shingo ya uzazi, kansa ya mapafu, rectal carcinomas, hepatocellular carcinomas, kansa za kichwa na shingo, na lymphomas.
. Toxoplasmosis (ugonjwa unaoshambulia ubongo).
. Tuberculosis (T.
dalili za ukimwi
Vipimo Vya UKIMWI
Ili kugundua kama mtu ana virusi vya UKIMWI au la, damu hutolewa na kupimwa kutumia vipimo maalumu kwa virusi vya IKIMWI. Kama virusi hivi vikipatikana, majibu huitwa “Positive”. Damu ya mgonjwa huyo hupimwa zaidi ya mara moja kabla ya kumpa mgonjwa majibu ya positive.
kuzuia ukimwi
Mgonjwa aliyegundulika kuwa positive hushauriwa kuchukua vipimo vingine ili kuona virusi hivi vimesambaa kwa kiwango gani na kujua ni lini mgonjwa aanze tiba. Ni vizuri mtu kuchukua tahadhari ya kupima mara baada ya kuwepo kwenye mazingira hatarishi ya UKIMWI kwani ugonjwa huu ukigundulika mapema zaidi
uwezekano wa tiba kufanikiwa unakuwa mkubwa zaidi. Inachukua kiasi cha wiki tatu hadi miezi mitatu baada ya maambukizi, virusi hivi kuweza kuonekana kwenye vipimo. | #Friend